Kuna dimensions ngapi?

Kuna dimensions ngapi?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Tuchukulie mfano wa shuka. Uzi uliotumika kushona shuka ni 1 dimension. Ukiurefusha unaweza kufika mamia ya mita kwa urefu. hata mwisho wake unaweza usiuone.

Shuka lililoshonwa ni 2 Dimension. Linatoshea kwenye kitanda cha tano kwa sita. Ukilikunja hilo shuka linakuwa 3 dimension. Linakuwa kafungu kadogo ka kutosha ndani ya droo la kabati. Lakini kwenye 3dimension kunakuwa na 2D na 1D.

Sisi tunajua mwisho 3 dimensions. Je kuna zaidi ya tatu? Shuka linaweza kuwa dimension ya nne na likawa dogo kiasi unaweza kuliweka mfuko wa shati? au likawa dimension ya kumi kiasi kwamba likawa halionekani hata kwa microscope? Inawezekana tunauo ulimwengu wetu mkubwa sana sababu tunauona katika 3D.

Lakini kumbe upo kwenye 10D na ukubwa wake hauzidi hata punje ya mchele.
Kuna uwezekano wa uwepo wa dimensions zaidi ya 3?
 
Back
Top Bottom