Kuna foleni kubwa Mlandizi hadi Chalinze, zaidi ya masaa matatu magari hayatembei

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Nipo Vigwaza, Mkoa wa Pwani natokea Dodoma. Kuna foleni kubwa kwa zaidi ya saa mbili sasa, na magari hayasogei kabisa. Foleni inaanzia eneo la Mlandizi hadi Chalinze, magari yanayotoka Dar es salaam hayasogei, na yanayotoka Morogoro nayo ni hali hiyo hiyo.

Naambiwa kuwa kero hii imekuwa kubwa tangu jana na leo. Maroli yameziba njia zote, hivyo hakuna anayepita.

Barabarani sioni jitihada za traffic kusaidia magari kuweza kutembea, tumekwama hatuelewi shida nini. Foleni tokea saa saba mchana imeganda.

Natoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia changamoto hii kwa haraka, kwani inaathiri muda wa watu. Kwa sasa, mtu analazimika kutumia zaidi ya saa saba kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam.
 
Unasema hapo tumetokqa kituo cha Loliondoo tokaa saa 1810pm naitafuta kwa.mathias kama sio kwenda kwa mkwe ningerudi acha tu ana bdayake mwamba nisipokuwepo keki haikatwii

Vumuliq tu.mkuu nakama umepanda basi chexesha miguu kidogo usipatr ganzi kama mm 😄 🤣 😂
 
Hapo maeneo ya Ruvu wamemaliza kujenga kile kipande cha lami kweli?

Kuna siku nilikutana na 'kitasa'nilikuwa natoka mkoa, ikabidi nikatize maporini kutafuta short cut huku bodaboda ananiongoza hadi nikatoboa karibia na daraja la reli...

Lakinkkulikuwa na kitasa hakuna mfano Ruvu Chalinze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…