Kuna haja gani ya kuendelea kufanya kaguzi za Serikali za mitaa iwapo matokeo yanawekwa bench?

Kuna haja gani ya kuendelea kufanya kaguzi za Serikali za mitaa iwapo matokeo yanawekwa bench?

nickodemus

Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
7
Reaction score
0
Kila mwaka Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Serikali anafanya ukaguzi na kutoa taarifa za kitaalamu. Matokeo yake ni ya wazi, na maoni yake ya kitaalamu kuhusu namna ya kurekebisha upotevu ama matumizi mabaya ya fedha za Serikali huwa ni lulu. Mara nyingi huwa yanafanya habari kubwa kubwa kwenye magazeti.

Lakini mara nyingi baada ya hapo, huwa yanawekwa kando. Kwa taarifa yako kwa miaka mitano iliyopita matumizi yenye maswali kwenye ripoti ya Mkaguzi yameongezeka toka Tsh 9 bilioni mwaka 2005/06 hadi Tsh 122 bilioni mwaka 2009/10. Na bado hakuna aliyewajibishwa.

Sasa tufanyeje?
 

Attachments

Back
Top Bottom