Mnanguliti
JF-Expert Member
- Apr 16, 2023
- 490
- 1,351
Habari zenu ndugu wana jukwaa letu pendwa.
Kama mada inavyojieleza ukiangalia mambo yanavyoendelea nchini unaona kabisa kuna kila sababu ya chama cha mapinduzi kuwekwa likizo maana hawana mbinu tena za kuliendeleza taifa hili. Nina sababu zifuatazo kuisupport hoja yangu katika hili.
1. Chama cha mapinduzi kimeshindwa kabisa kulibadilisha taifa ili lionekane la kisasa pamoja na kuwa na rasilimali nyingi tulizopewa na Mwenyezi Mungu ikiwemo, ardhi yenye rutuba, misitu, mapori, wanyama wa kila aina, madini ya kila aina, bahari ya hindi, maziwa mengi yanayopatikana nchini, mito inayopatikana karibia kila mkoa au angalau kila kanda ya kiutawala ina mto au mito mikubwa.
Pamoja na uwepo wa rasilimali zote hizo nchi hii bado imekuwa nyuma ya nchi ambazo hazina rasilimali anuwai. Viongozi wanaotokana na chama hiki kikongwe barani Afrika wamekuwa wapigaji kiasi kwamba taifa linaonekana kama halina mwenyewe yaani kila rais wa nchi anayechaguliwa kupitia chama hiki amekuwa mstari wa mbele kulihujumu taifa na kujilimbikizia mali yeye pamoja na watu wake wa karibu. Hali hii imelifanya taifa liwe shamba la bibi, kuna wakati ukifikiria mpaka unaona hata vyombo vyetu vya dola ni kama vimebariki hili taifa lichezewe kama halina mwenyewe.
2. Uuzwaji au ubinafsishaji wa rasilimali zetu unaofanywa na viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi umelifanya pia taifa lisijue kipi linakisimamia mfano kuondolewa kwa wananchi wa Ngorongoro na Loliondo ili kumpisha mwekezaji na kupewa wageni kwenye bandari zetu ni kama tumeporwa rasilimali zetu muhimu sana kama taifa. Wamasai wanaishi maisha ambayo hawakuyaishi kabla ili tu kuwaachia wanaccm wafanye ujinga kwenye taifa letu.
3. Kutekwa,kupigwa, kuumizwa, kungo'lewa, meno, kupigwa risasi na kuuawa kwa wakosoaji wa serikali ni janga jingine kubwa ambalo linanifanya nione hiki chama kimelewa na kimepoteza legitimacy ya kuongoza taifa maana hivi sasa ni kawaida sana mtu kukamatwa na vyombo vya usalama na kifanyiwa unyama wowote ili tu usiwakosoe ccm yaani utadhani hawa watu walizaliwa peke yao nchi hii. Kuna haja wananchi au watanzania kwa umoja wetu kukipumzisha hiki chama ili waingie wengine wenye maono tofauti ya kulifanya taifa letu liwe bora. Naamini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikiamua kutafuta mtu mzalendo na kumpandikiza kwenye chama chochote cha siasa tofauti na Ccm na ikawekwa fair ground ya wagombea tutapata kiongozi thabiti ambaye angalau ataondoa minyororo ya hiki chama ambacho kwa sasa lomekuwa ni kabila ambalo mtu hata awe kiongozi mzuri kiasi gani asipotokea kwenye kabila hili dhalimu la Ccm hawezi akapewa nafasi nyeti.
4. Ufisadi, wizi na mambo mengine ya kulihujumu taifa umekuwa mkubwa kiasi kwamba taifa kwasasa linajiendea tu, kuna wanasiasa wanamiliki mali nyingi sana zilozotokana au zinazotokana na kuliibia taifa na viongozi wa juu ni kama hawaoni kama kuna shida yaani tukisema tuweke rekodi ya watu 20 au zaidi ya matajiri wa Tanzania watakaoongoza ni wanasiasa wa chama cha mapinduzi na katika orodha ya hao 20 anaweza asiwepo mfanyabiashara hata mmoja sema haya majitu yanaficha sana taarifa zake.
Kwasababu hizo chache na nyingine nyingi ambazo sijaziandika nawaomba sana watu wa usalama wa taifa, jeshi la wananchi na vyombo vingine vya dola vilihurumie hili taifa maana hili taifa litakuwepo hata baada ya wajukuu wa wajukuu zetu. Wao kwa mafunzo waliyoyapata na viapo walivyokula ni taifa kwanza masilahi binafsi baadaye. Nimevitaja vyombo hivyo kwasababu najua kabisa vyama vya upinzani ni kama vimezidiwa nguvu na vina mapandikizi mengi mno ya hili lichama lakini pia watu wengi wa upinzani wanafika bei.
Naamini hatujachelewa sana TISS na TPDF liokoeni hili taifa litamalizwa na haya maccm.
Naomba mnisamehe sana vyombo tajwa kama nimevuka mipaka ina kwakweli inatia hasira sana taifa letu kuwa mali ya watu wachache.
Ahsanteni sana!!