Kuna haja sasa ya kuliangalia suala la Ubingwa kwa macho makali

Kuna haja sasa ya kuliangalia suala la Ubingwa kwa macho makali

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Nitoe pongezi kwa team ya Yanga, Azam na hata Simba kwa kushika nafasi walizoshika katika ligi na pia team nyingne zilizofanikiwa kuendelea na ligi mwakani. Kwa tema zilizoshuka nizipe pole ila hakukuwa na jinsi ni lazima tu team zingeshuka ndivyo uratatibu ulivyo wengine washuke ili wengine waweze kupanda.

Lililonileta hasa ni kiasi cha pesa zinazopatikana kwa bingwa mshindi wa kwanza wa pili na watatu katika VPL. Kiuhalisia ni kiasi kidogo na cha kusikitisha sana, pamoja na kwamba wengne watasema lengo la ligi si team kupata pesa lakini jaman tuangalie kiuhalisia. Pamoja na kuwa tu ni tittle lakini tuangalie pia faida ya kupata kombe ukiacha ile ya kwenda kucheza mechi za kimataifa.

Ni sawa mshindi anakuwa mwakilishi wa mashindano ya kimataifa na pia anakuwa na kombe lakini je anapokea kiasi gani kama zawadi? Sidhani kama inazidi mil 100. lakini ukiangalia maandalizi ya michuano hi na purukushani zake ni zaidi ya pesa hizo anazopata mshindi.

Kama mshindi wa Miss Tanzanis tu ana uwezo wa kupata zaidi ya mil 50 hatuoni kuna haja ya kuwashawishi wafadhili wa ligi hii kuongeza kiwango cha mshindi wa kwanza na wa pili?

Angalau pesa hizo zinazopatikana ziisaidie team husika kwenye maandalizi ya kimataifa? Hatuoni hii italeta hamasa kubwa hata kwa hzii team ndogo ndgo zisizo na wafadhili au matajiri kupigana kufa na kupona ili waweze kupata pesa ambazo ziwasaidia kwenye kulipa mishahara au usajilina pia mashindano ya kimataifa? Hii ingeleta ushindani mkubwa zaidi hasa kwa team ambazo ni maskini ukilinganisha na team matajiri.

Jamal Malinzi ungetumia nafasi hiii sasa kuweza kukaa chini kuongea na wafadhiri wa ligi hii ili kuongeza dau angalau hata pesa ya mshindi ifike 300 au 500 kitu ambacho naamini kinawezekana. na katika hili yapamanishwe makampuni mengi ili atakayekuja na dau kubwa ndo apewe ligi . Faida tunajua zipo ikiwepo kutangaza bidhaa husika kwa mwak mzima n.k.

Jamani ili ligi ipate heshima ni pamoja na pesa za kutosha kwa washindi. Naomba hli pia likufikie Jamal Malinzi na TFF kwa ujumla.
 
nasikia mshindi wa kwanza anaambulia m70 tu, kama ni kweli basi ni kiasi kidogo mno, bora iwe 300M-500M kama mleta mada anavyoshauri
 
ni ujumbe mzuri lakini kwa viongozi wetu mmmhhh!!!!!!!...
 
tatizo sio malinzi wala tff ni upeo mdogo wa viongozi wa vilabu ndio wanafanywa waendelee kunyonywa mpaka pale watakapozinduka ndio mambo yatabadilika ikwani wanaingiza pesa nyingi lakini hawajielewi
 
Back
Top Bottom