Kuna haja ya Elimu zaidi Kwa wajasiriamali na wawekezaji wadogo wadogo.

Kuna haja ya Elimu zaidi Kwa wajasiriamali na wawekezaji wadogo wadogo.

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Habari za jioni jamii forum

Kazi ni maisha,kila hatua na kila siku tunahitaji ubunifu mpya kwenye mishe zetu ikiwa ni njia ya kujikwamua na kuuacha umaskini haswa Kwa sisi watu wa kipato cha chini.

Lakini je,tuna elimu ya kutosha Kwa tuyafanyayo,au tunayoyaanzisha?

Au ni tamaa na kuiga tu ikiwa huna utaalamu na ujuzi wa kutosha?

Umeamua kulima,je Una utaalamu na hilo eneo kuhusu muda wa kuandaa shamba ,viuatilifu na uhudumiaji wa shamba?

Je,unaweza kufuga ng'ombe,mbuzi,kondoo na nguruwe (haswa mikoani) Kwa kufuata utaalamu,yaani madawa,chakula sahihi cha mifugo au unaiga kwakuwa fulani anafuga?

Una uwezo wa kutosha (kipesa) kuhudumia mifugo?

Kutesa kiumbe nidhambi kubwa.

Pichani ni nguruwe wakiwa kwenye Banda lao lisilofanyiwa usafi,na pia wanaonekana hawazingatiwi kwenye chakula na madawa.

Nimesikitika Kwa kweli.
 

Attachments

  • 20250208_153526.jpg
    20250208_153526.jpg
    115.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom