Kuna haja ya kichuri kuanza kuuzwa supermarkets na kwenye maduka makubwa

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Kichuri (African Sauce) ni kiungo kitamu cha nyama haijawahi kutokea. Unaweza kula nyama choma mbuzi mzima.

Awali nilidhani kichuri inaliwa tu kanda ya ziwa hasa Mara ila baada ya kutembelea mikoa mingi ya Tanzania nimegundua Watanzania wengi wanapenda kichuri hasa kula na nyama choma.

Nashauri sasa ni wakati muafaka kichuri kianze kuuzwa supermarkets na kwenye maduka makubwa ya chakula. Pia baadae tuanze ku-export kichuri huko Ulaya tutapata pesa nyingi sana za kigeni.

Ni wakati sasa serikali au mamlaka zinazosimamia machinjio yote nchini kuhakikisha kunakuwa na utengenezwaji wa kichuri kwa kila mbuzi au ng'ombe anayechinjwa ili kikauzwe supermarkets.

Tupende vya kwetu tuthamini vya nyumbani.
 
Naomba recipe ya hiyo kitu kwanza kabla sijawaza kuitumia,maana masaini wanatumia hadi mavi-mavi ya kwenye utumbo wa mbuzi na ngombe kunakshia nyama choma,vitu vingine ni haramu tu hakuna mbadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…