Ngurubhe
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 1,840
- 1,049
Mim ni shabiki wa Yanga lakini pia ni Mwanamabadriko kisiasa.huwa mara nyingi siku kama ya leo nashindwa kuvaa sare za Yanga, kwani huwa najihisi navaa rangi inayofanana na ya ccm,niseme kweli huwa siipendi CCM.Ni shabiki mdogo sana kiasi kwamba hata sijawahi kuonana na kiongozi yoyote wa yanga, pengine ningekuwa shamupa dukuduku langu ili wakikaa huko vikaoni walijadili hili.
Nasema hivi kwa sababu najua nguvu ya rangi katika kufikisha ujumbe,wapo wanaosema sababu za kihistoria ati ndio maana kko hivyo.
Kwangu sababu hizo naona hazina mashiko kwani michezo ina nafasi ya kutuunganisha bila kujali itikadi zetu,sasa kama nikiona rangi inayofanana na chama fulan cha kisiasa nashindwa kujizuia kuichukia team pia.Na nibora nikashabikia team kuliko chama...
Naamin kuna siku kuna mtu atapitia uzi huu na kulijua kama ni moja ya tatizo la kisaikolojia katika vichwa vya baadhi ya watu wenye mapenzi na Yanga lakini muda huohuo hawana mapenzi na ccm then wanajikuta wanaichukia CLUB YA YANGA bila kujua sababu.
Itakuwa ni jambo jema kwa ccm kama mtu ataanza na kuipenda yanga,then baadae akapenda ccm..lakin mim naamin na wengine wengi tunaipenda yanga lakini hatuipendi ccm..na ningependa kuvaa jezi za timu yangu lakini sio hizi!!....nichekeni lakin huo ndio mtazamo wangu....
kama upo simba nakupenda pia kwani wew utabaki kuwa mtani wangu tu.....