Kuna haja ya kubadili msimamo wa kauli ya serikali kuhusu bei ya mahindi

Kuna haja ya kubadili msimamo wa kauli ya serikali kuhusu bei ya mahindi

Killing machine

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
2,052
Reaction score
2,995
Habari zenu wakuu,

Kama mnavyo jua serikali yetu Haina misingi imara ya ajira kwa watu wake hivyo kutegemea sector binafsi kutatua angalau tatizo la ajira inchini

Na tunapo zungumzia sector binafsi ni pamoja na viwanda vidogo vidogo vinavyo milikiwa na wakulima pamoja na wafanya biashara wakubwa na wadogo

Hapa majuzi serikali yetu pendwa ilitangaza rasmi kununua mahindi kwa bei za 700 per kg kwa mjini lakini 600 per kg kwa vijijni

Lengo la kuweka 600 per kg kwa vijijni ni ili hiyo 100 ya juu isaidie kusogezea mzigo mpaka mjini ikiwemo upimaji upakiaji ushushaji na ushuru

Kwahilo naipongeza serikali yetu kwa kuwalinda wakulima na wafanya biashara kwa wakati mmoja lakini pia hata ajira kwa vijana wakazi za ukibega nk

Lakini Changa Moto nikwamba mfanya biashara mwenye mtaji mdogo wa kuanzia 5 mpaka 10 mil anapo enda kijijini/shambani ananunua mzigo 10 tones mpaka 20 tones

Anausafirisha mpaka sokoni ambapo serikali Ina nunua mzigo huo kwanza una angaliwa quality yake Kama nzuri/mbaya

baada ya hapo una chekechwa Kisha unapakiwa kwenye mifuko special na muuzaji anaandikisha kgs zake na kusubili mpaka atakapo itwa na mawakara hao kuichukua pesa yake kumbuka mpaka atakapo itwa

Zoezi ambalo hufanyika kwa wiki mbili na zaidi kwa siku za mwanzoni lakini huchukua zaidi ya mwezi kwa siku za mbeleni kitubambacho Kina gharimu muda kwa mfanya biashara

Lakini pia uchekechaji wa mahindi una athali kwa mfanya biashara

kwa mfano una nunua gunia lenye ujazo wa 100 kgs unapima kwa pesa unapakia kwa pesa una safirisha kwa pesa unalipia ushuru na unakuja kulishusha kwa pesa

Baada ya kulichekecha Lina bakiwa na 80kgs hapo unakuwa umepoteza 20kgs Mara 200 bags ambayo NI sawa na 4000kgs mara 700 unapata hasara ya 2800000 kwa gunia 200

Kitu ambacho nitofauti na masoko mengine ya kenya,Zambia,lwanda na Malawi na mengine ya ndani Kama mwanza morogoro nk

Kwenye hayo masoko hapo juu Wana angalia mahindi Kama mazuli unalipwa pesa yako hapohapo

unaludi shambani kuchukua mzigo mwingine haraka na una tengeneza faida kubwa kwa mda mfupi na sahihi

Lakini mfumo wa serikali yetu wa ununuzi kwanza una punguza faida,pili unaghalimu mda hasa kwa wafanya biashara wenye mitaji midogo

Lakini pia unauwa mzunguko wa kibiashara nahivyo kupelekea watu wengi kuendelea kulundikiwa mzigo wa liba kwenye mabenki yetu na weza kusema/kuuita ni mfumo firisi

Vilevile mfumo huu wa serikali unauwa ajira kwa wafanya kazi/vibega na wafanya biashara pamoja na wasafirishaji/wamiliki wa magali mipakani na ndani ya inchi.

Kingine mfumo huu una poteza mapato ya serikali mipakani kupitia ushuru balabalani mpaka ukataji wa vibali.

Nimetembelea kasumuru kule kyela, na tunduma kule songwe masoko ya ndani ya mazao kiukweli Hari sio nzuli watu Wana lalama Hari ni ngumu.

Kwani serikali imezuia mahindi yasiuzwe kwenye masoko mengine isipokuwa wao lakini inachelewesha pesa na liba kwenye mabenki Zina ongezeka.

Ushauri wangu juu ya tamko la raisi nikwamba.

Serikali ingeruhusu watu kuuza mahindi popote watakapo kwa kufuata Sheria na taratibu zili zopo.

Huku na wao wakiendelea kununua mahindi pasipo kuathili Maisha ya watu wengine au sectors nyingine.

Kinyume na hapo Kuna hatari ya watu kuanza kulala saa 12 za jioni kwani vijana hawana kazi na family zao Zinahitaji chochote.

Kuna hatari ya watu kuuziwa majumba/kunyanganywa dhamana zao na mabenki.

Na la mwisho msisahau kauchaguzi kame kalibia kwahiyo msiji sahau sana.

Ukijumlisha nahii mizigo ya tozo tuliyo nayo sijui.

Pia, soma:

1) Kuelekea 2025 - Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa mia 700 kwa kilo

2) KERO - Serikali isikie kilio cha wakulima wa zao la Mahindi wa Nyanda za Juu Kusini
 
Serikali la CCM lipo kurudisha nyuma watu, hawana akili ya maendeleo ni majizi matupu
 
😁😁😁 serikali ya TZ ipo kwa ajili kukwapua pesa za wanyoge
 
Back
Top Bottom