Uchaguzi 2020 Kuna haja ya kuchagua wabunge hamahama?

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
259
Reaction score
292
October 2020 kuna uchaguzi mkuuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

2015-2020 baada ya uchaguzi kuisha baadaye tulishuhudia wabunge na madiwani wakihama vyama vyao na bahati mbaya sana wamelitia taifa hasara kwa faida zao binafisi.

Tumeingia gharama za kurudia uchaguzi katika maeneo mengi fedha ambazo zingeweza kufanya kazi nyingine. Je, kuna haja ya hawa watu wakiomba kuchaguliwa tena wachaguliwe tena?

Je, watu hawa hawatahama vyama vyao tena tukaingia gharama za kurudia uchaguzi tena?
 
Unaona hao wabunge ndio wanalitia hasara taifa? Jiulize ni nani anayehamasisha hao wabunge kuhamahama kisha kukimbilia kutangaza chaguzi ndogo? Unafikiri wanaamua wenyewe kuhama hivi hivi bila motisha yoyote? Nani anayetoa pesa kwa ajili ya chaguzi hizo? Inamkera? Huyo ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia mwenendo wa wanasiasa nchini. Ndiye anayeweza kuzuia tusipate hasara hizi za kijinga - AKIAMUA.

Kifupi ni kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa Tz hauwezekani.
 
Na

Nadhani ingetungwa sheria anayehama asigombee uwakilishi wowote.Huwezi kutangaza sera za chama fulani ukachaguliwa kwa sera hizo.kisha kabla yakumaliza kipindi chako ukaanza kuziponda sera hizohizo ulizo chaguliwa nazo
 
Mkuu sana kilasi Mkuu nakuunga mkono kwa 100%
 
Je waliotimuliwa bila makosa na Wao wanaingia kwenye hoja yako mkuu?
 
Mimi nasubiri kabla sijakujibu unambie kama tunayo Katiba ya chama chochote hapa Tz inayosema hakuna mbunge wake kuhama. Hapo ntakupa support yangu. Lakini kama ni free then just leave free to free itself freely.
 
Unaona hao wabunge ndio wanalitia hasara taifa? Jiulize ni nani anayehamasisha hao wabunge kuhamahama kisha kukimbilia kutangaza chaguzi ndogo? Unafikiri wanaamua wenyewe kuhama hivi hivi bila motisha yoyote? Nani anayetoa pesa kwa ajili ya chaguzi hizo? Inamkera? Huyo ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia mwenendo wa wanasiasa nchini. Ndiye anayeweza kuzuia tusipate hasara hizi za kijinga - AKIAMUA.

Kifupi ni kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa Tz hauwezekani.
Angeweza zuia hasara Kama Ingekuwa ni kinyume chake yaani wanahamia upinzani toka ccm hapa suala la gharama lingeonekana.
Chochote kinachohusu kuuwa au kuumiza upinzani suala la gharama huwa halitazamwi
 
Kama unahama usiogombee kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom