Kuna haja ya kufundisha somo la economics na entrepreneurship kwa lazima kuanzia ngazi ya sekondari

Kuna haja ya kufundisha somo la economics na entrepreneurship kwa lazima kuanzia ngazi ya sekondari

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
Habari zenu wakuu, ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya tele. poleni kwa mlio na walakini kwa namna yoyote ile.

ama baada ya salamu, nina hoja ambayo ningependa tuizungumzie kwa pamoja kama watanzania ili kuliokoa taifa na janga la ukosefu/upungufu wa ajira.

MAIN TOPIC ambayo ningependa tupenane mawazo ni kuhusiana na ufundishwaji wa masomo ya uchumi na ujasiriamali kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya sekondari mpaka ngazi ya chuo kikuu (degree ya kwanza)

ndugu wadau, mimi mleta mada ni mwanafunzi wa mwaka wa pili, higher learning fulani hapa Tanzania, na nimeona si vibaya tukaongelea mustakabali wa maisha ya vijana wetu ambao wengi wao huamini katika kuajiriwa sana badala ya kutafuta mbinu ya upande wa pili ambayo ni kujiajiri na kuondokana na tatizo la kukaa mtaani kusubiri ajira.

wakuu, kwa hali ilivyo sasa, kuna wahitimu wengi sana mitaani na wengine humwagika kila siku mitaani kusaka nafasi mbali mbali za ajira ambazo zinakuwa limited. kama mnavyojua, elimu ya kitanzania haimjengi muhitimu katika kujitegemea, bali inamfanya muhitimu ategemee dirisha moja tu ambalo ni ajira kutoka katika ofisi mbali mbali ambazo ni chache sana kwa hali ilivyo.

hivyo, mimi kwa maoni yangu, nashauri serikali ibadili mitaala yake na kuweka somo la uchumi pamoja na ujasiriamali kuanzia ngazi ya sekondari mpaka vyuoni ambapo wanafunzi watayasoma hayo masomo kama core subjects. Tena ikiwezekana, somo la finance nalo liongezwe katika orodha. hii itaweza kumjenga mhitimu yeyote yule awe ni wa kidato cha nne, sita ama yule wa degree kuweza kuja kutengeneza biashara yake mwenyewe badala kuja kutegemea nafasi chache za ajira ambazo haziwatoshelezi. hii itaondoa sana tatizo la ajira kwa nchii hii ambayo ina uchumi unaokua.

ndugu wadau, kwa wale ambao mlisoma enzi hizo, mnakumbuka sana somo la ELIMU DHIDI YA UKIMWI (EDU) lilivyokuwa la msaada mkubwa sana kwa wanafunzi wa shule za msingi na elimu kwa ujumla, japo sikulikuta, lakini naamini waliolisoma walinufaika sana na hilo somo, sasa ni wakati mbadala wa kuanzisha kitu kingine.

somo la economics and entrepreneurship, naomba lingechukua nafasi ya General Studies lakini ili kuliongezea ukali zaidi, performance yake ipandishwe ili wanafunzi watambue umuhimu wake kwao kwa vile wengi wao hudharau masomo ya subsidiary. ama, liondolewe kabisa sifa ya subsidiary, na lipewe credit kama masomo mengine ili liwe na umoto moto.

ndugu wadau, haya ni maoni yangu tu katika kupambana na tatizo la ajira katika nchi yangu ya TANZANIA. INASHANGAZA SANA KIJANA ANAKUWA NA KAMA SHILINGI MILIONI MOJA AMA PESA YOYOTE ILE HALAFU ANAULIZA NINI CHA KUIFANYIA. HILI SI KOSA LAKE, NAHISI NI KOSA LA SYSTEM NZIMA YA ELIMU. MUDA WA KUBADILIKA NI SASA.

Asanteni na karibuni kwa maoni.
 
Mtizamo wangu: wanafunzi kuanzia sekondari wawezeshwe mambo ya msingi kabisa kuhusu uchumi na ujasuriamali.
Kuwezeshwa huko kufanyike kupitia semina, machapisho, ...ambayo yatawafanya wanafunzi wenye nia kujifunza.
Kufanya kama somo la lazima haitosaidia, kwani, madhara ya cenralised curricular, yatazuia kufanikiwa kwa somo husika.
Wanafunzi wanapaswa kujengewa misingi ili wajifunze kwa uhuru, na kudadisi juu ya baadhi ya mada za somo husika.
 
ni kweli kabisa ndugu wapewe somo hilo,hata waweke kama option tu watakao lisoma litawasaidia sana,
 
Kujua masuala ya uchumi sio option ni lazima.
 
Back
Top Bottom