Kuna haja ya kumshtaki mahakamani Meya wa Manispaa ya Moshi

Kuna haja ya kumshtaki mahakamani Meya wa Manispaa ya Moshi

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Huyu Meya alifikiri ni sifa kuwaamrisha watu waliohudhuria mkutano wa baraza la madiwani wa manispaa hiyo kwa mawazo yake ya kijinga kuwa ilikua makosa kuvaa Barakoa wazive na kama hawavui wachukuliwe hatua. Madai yake ilikua eti manispaa haina ugonjwa wa Corona. Kwani Barakoa inakinga Corona pekee?

Huu ulikua ni utovu wa nidhamu pamoja na ukaidi wa meya huyu juu ya Afya za watu. Kama yeye aliamua kutovaa basi angebaki yeye na sio kutoa amri za hivyo zilizojaa sifa.

Sasa tunafikiria kua kuna haja ya kumshtaki huyu Meya kwa kuhatarisha afya za watu makusudi huku akikiuka maagizo na maelekezo ya wataalam wetu wa Afya kua ni lazima kila mtu achukue tahadhari.

Hii amri yake ni kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu pia. Kila mtu anayo haki yake ya kimsingi kujilinda na maradhi na huu pia ni wajibu.
 
 
56853.jpg
 
Mkimshitaki mtakua mnamuonea,watu wazima wanaojitambua na kuzijua kanuni za afya watalamishwaje kuvua barakoa na layman kama huyo meya?ingekua ni jeshini labda maana kule ni kutiii tu basi.
 
Back
Top Bottom