Kuna haja ya kupitia asilimia za mapato TFF inavinyonya vilabu

Kuna haja ya kupitia asilimia za mapato TFF inavinyonya vilabu

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Wadau wa soka naamini mmeona mgawanyo wa mapato katika Mechi ya Simba na Yanga. Binafsi naiona TFF inavinyonya Vilabu kwani kuna mapato yanaitwa

1.TFF
2.TPLB
3.GHARAMA ZA MECHI

Binafsi naona mapato ya TFF ndio yangegawanya kwa TPLB na Gharama za Mechi. Tukumbuke TFF imeshindwa kuvipatia vilabu Wadhamini kwa hiyo Vilabu vinajiendesha kwa kutumia hayo Mapato, hakika TFF inavinyonya Vilabu ndio maana Migogoro ya kufukuzana haiishi pale TFF.

Tunaiomba Serikali kama inadhamira ya dhati kuviinua vilabu basi TFF ipunguziwe asilimia ya Mapato. Na kama TFF inataka fedha ibuni vyanzo sio kutegemea Mapato pia TFF kuna Fedha inapata kutoka FIFA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta Uzi nakuunga mkono 100%, Hawa tff na wenzake wanavinyonya vilabu.
 
Hivi timu zetu zikiwa na viwanja vyake, hayo makato ya kipuuzi zaidi ya VAT yatatoka wapi?
 
Watu wanakuza vitambi tu...anyway tukisema sana tutaambiwa tuna wivu wa kike.
 
Hivi timu zetu zikiwa na viwanja vyake, hayo makato ya kipuuzi zaidi ya VAT yatatoka wapi?
Wataingiza tu. Afu huko nako kutakuwa na gharama za makomandoo

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
TFF na Board ya ligi ni hao hao.
Kama kuna VAT anapata mwenye uwanjani,gharama za mechi zinatoka wapi tena?
BMT na DRFA wanachukua mgao kwa lipi?
Kuna ka harufu ka upigaji hapo
 
Wataingiza tu. Afu huko nako kutakuwa na gharama za makomandoo

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Mkuu, hizo za makomandoo ni za club kwa matakwa yao. Hata za kamati za ufundi humo humo. Ni za wajanja wachache.
 
Tatizo ninaloliona hapa ni kuweka mlolongo wa makato yasiyo na maana yoyote na yanachukua asilimia kubwa. Hata timu ikijenga uwanja Sidhani kama utakuwa mkubwa sana kama ule wa taifa. Mfano uwanja wa chamanzi hata bila makato Hauwezi kupata pesa nyingi kama ukicheza taifa na ukatwe. Uwanja wa azam complex unachukua watazamaji 7000 tu. Kwa simba na yanga ili wajikomboe labda wajenge uwanja wenye kuingiza mashabiki wasiopungua elfu 40.
 
Hata viwanja vya kuanzia watu 20,000 is haba kwa timu zetu hizi . Ukiondoa makato ya dhulma, wanaweza kupata hela za maana. Lakini upuuzi wa TFF, bodi ya ligi, DRFA viondoke. Hata ikibidi kwenda FIFA. Nahisi ni upuuzi wa Bongo tu
 
Bmt wana ruzuku,Pia nadhani vat ilitosha cos ni serikali hiyohiyo
 
Azama alikuwa analazimishwa kucheza National Stadium mechi za nyumbani vs Simba na Yanga walishaacha?
 
Back
Top Bottom