Kuna haja ya kuwepo kwa adhabu ya kifo

Kuna haja ya kuwepo kwa adhabu ya kifo

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Kumekua na matukio mengi sana kwa watu kuuliwa maeneo mbali mbali nchini kuanzia mwishoni mwa mwaka 2021 hadi leo hii kila siku yanaibuka mauaji sababu zikiwa wivu wa mapenzi,dhuluma,tamaa ya mali na hasira.

Binafsi naona kwa hali ilivyo sasa uhai wa binadamu umekua kitu cha kuchezea kama kumkanyaga sisimizi licha ya nchi nyingi kuipinga adhabu hii na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu naona kwa sasa ni muda wa kuanza kuitumia hii adhabu matukio ni mengi kila siku kila kona ya nchi.

Naona watu hawaogopi kwenda condemn wanajua watakaa badae watabadilishiwa adhabu na kua kifungo cha maisha sasa ni muda wa kuanza kuitekeleza adhabu hii ili kupunguza ukatili huu.
 
Ipo, sema haitekelezwi, shida inakuja , wanaohukumiwa kifo si wenye hatia, bali ni wale wasio na pesa ya kuhonga. Ditopile Mzuzuri unamjua?! Andrew Chenge unamjua? Wote waliua...

Napinga hukumu hii kwa nguvu zote, maana masikini wengi watanyongwa, innocent /guilty.

Pia kumbuka, maisha ya Condemn ni kama Jehanam, sio free ride
 
Psycopath marekani wapo wengi. Licha ya sheria za hukumu ya kifo kuwepo. Bado watu wanauana tu.
Isiwepo Kwa nchi yetu.
 
Watu wanatembea wakiwa hai lakin walishakufa ndani kwa ndani
 
Haja ipo. Sema tu Rais aondolewe mamlaka ya kuidhinisha adhabu ya kifo. Anajua nini juu ya adhabu na sheria?
 
Ipo, sema haitekelezwi, shida inakuja , wanaohukumiwa kifo si wenye hatia, bali ni wale wasio na pesa ya kuhonga. Ditopile Mzuzuri unamjua?! Andrew Chenge unamjua? Wote waliua...
Kuna classes za mauaji, Ditto aliua ila ilikua ni manslaughter, hakua amedhamiria kumuua yule dereva, ilitokea bahati mbaya tu akaghafilika, the same na Chenge, hizo bahati mbaya mtu kufungwa maisha ama miaka kadhaa nakubaliana nazo kabisa.

Hapa tunaongelea pre meditated murder, umepanga, umeandaa kila kitu na ukadhamiria kuua, huyo hana sababu ya kuhurumiwa, lazima auwawe na yeye.
 
Psycopath marekani wapo wengi. Licha ya sheria za hukumu ya kifo kuwepo. Bado watu wanauana tu.
Isiwepo Kwa nchi yetu.
Asikudanganye mtu, adhabu ya kifo inapunguza matukio ya mauaji, ndio maana wauaji wengi wakiambiwa watahukumiwa kifo basi wanaomba ku strike deals na waendesha mashtaka ili wahukumiwe kifungo cha maisha na sio kifo.

Halafu, Marekani sio majimbo yote yana adhabu ya kifo.

Wangekua hawaogopi kifo wasingekua wanaomba kuondolewa adhabu ya kifo badala yake wafungwe maisha.

Mtu ameua mwenzake kw akukusudia hana sababu ya kuishi.
 
Kuna classes za mauaji, Ditto aliua ila ilikua ni manslaughter, hakua amedhamiria kumuua yule dereva, ilitokea bahati mbaya tu akaghafilika, the same na Chenge, hizo bahati mbaya mtu kufungwa maisha ama miaka kadhaa nakubaliana nazo kabisa.

Hapa tunaongelea pre meditated murder, umepanga, umeandaa kila kitu na ukadhamiria kuua, huyo hana sababu ya kuhurumiwa, lazima auwawe na yeye.
Shida ndio ipo hapa, masikini wengi wanaofanya ‘manslaughter’ watanyongwa wakati walichofanya si ‘murder’, ila kwa unyonge wao, polisi wanapodai rushwa halafu huna / hutaki basi wanakukomoa na murder charges. Masikini wataishia kunyongwa kama mbwa!!
 
Binafsi nikiwaza tukio la kuuawa kwa Gema Haule(23) mhudumu wa gesti songea naona iwepo kumnyonga wenzako kwa kamba za viatu hadi kufa kwann wewe usinyogwe?

Tena wale wote wataothibitika wameua kwa kukusudia, wakaangwe kwenye karai kubwa la mafuta ya moto au wachemshwe kwenye pipa la lami au wawe wanakatwa kiungo kimoja kimoja kila siku...
 
Shida sio hukumu ya kifo mi nazan serikali ingeaza kukiaandaa kizazi kwa kupeleka masomo ya saikolojia shuleni ili mtu aweze kukabiliana na tatizo la kihisia
 
Shida sio hukumu ya kifo mi nazan serikali ingeaza kukiaandaa kizazi kwa kupeleka masomo ya saikolojia shuleni ili mtu aweze kukabiliana na tatizo la kihisia
 
IPO ILA UTEKELEZAJI

HAKI ZA BINADAMU UTAWAAMBIA NINI WAKUELEWE
 
Tatizo ni nyumba za ibada zimeacha kufundisha upendo nao wanafundisha tozo....toa sadaka tuuuuu ndo yamejaa kichwani mwa watumishi wa Mungu.Pia familia nyingi zimeacha maadili kila mmoja anajijali yy tunazalisha jamii mbovu sana ni miaka ijayo tutashuhudia zaidi ya haya tusipo badilikia.
 
Back
Top Bottom