Kuna haja ya Simba na Yanga kuja na wazo moja na kujenga uwanja wakatumia pamoja zinatia aibu

Kuna haja ya Simba na Yanga kuja na wazo moja na kujenga uwanja wakatumia pamoja zinatia aibu

Rais wetu Injinia Hersi na Bosi wake GSM walituahidi mchakato wa ujenzi utaanza mapema! Mpaka sasa hata sijui wamefikia wapi!! I wish wangetimiza ahadi yao kwa vitendo.

Haiwezekani timu ndogo kabisa zinajenga viwanja vyao viziri na kwa gharama ndogo! Halafu Yanga na Simba kila siku viongozi wanaleta porojo tu. Timu zimeanzishwa tangu miaka ya 1930's!! Lakini zinapitwa na timu za miaka ya 2000!! Aibu gani hii.
 
Mashabiki wa Simba na Yanga wanapenda mambo makubwa ila hawapendi kuwa sehemu ya kufanikisha mambo makubwa. Kulipia kadi ya uanachama tu mzozo. Mwingine utamkuta kavaa jezi feki huku povu linamtoka kwanini timu yake inasajili wachezaji wa Mwadui.

Kwa mastaa wanaoletwa kwenye hizi timu kiongilio kilitakiwa kianzie 20000 kwenda juu. Imagine unaenda kumuona Mvp wa Ivory Coast kwa buku tatu. Klabu zitaendelea vipi kama sio kuendelea kuwaaimbia nyimbo za mapambio Mo Dewji na Gsm?

Kiufupi Mashabiki wa Simba na Yanga hawana tofauti na mashabiki wa Hip Hop ngumu, kazi kusifia tu kwenye shoo hawatoki, albam hawanunui.
 
Yanga na Simba waondoe tofauti zao kwa muda wajenge Uwanja mkubwa sana na wautumie pamoja .

Waige kwa Ac Milan na Inter Milan , Birmingham city na Coventry, Lazio na Roma na vilabu vingine ....ifike mahali waone aibu .

Soma Pia: Yanga kujenga Uwanja wa kisasa eneo la Mto Msimbazi!
Halmashauri za wilaya na majiji nazo zilitakiwa kujenga viwanja vya soka ili hizi timu zitie nguvu kwenye kujenga viwanja vya kisasa vya mazoezi.

Viwanja vya kisasa vya mazoezi kwa Simba ya Yanga ni muhimu zaidi kwa wakati huu ambao zinawekwa kwenye mzani mmoja na vigogo wa soka la Afrika.

Hata huo uwanja unaotumiwa kama uwanja wa nyumbani wa AC Milan na Inter Milan, unamilikiwa na Manispaa ya jiji la Milan. Kama unaotumiwa na Lazio na Roma unavyomilikiwa na Kamati ya Olimpiki ya Italia, siyo hivyo vilabu.

Hivyo, kama manispaa ya Kinondoni wamejenga uwanja, kwanini hizi manispaa nyingine nazo zisijenge viwanja na tukaziacha Simba na Yanga zibaki kushughulikia viwanja vya ufundi.

Ova
 
Bora tusiwe na uwanja kuliko kushirikiana na Kolowizard.
 
Hebu niambieni hapa Bongo timu gani inamiliki uwanja wake, hakuna timu hata moja yenye uwanja wake. Msiwatie pressure Simba na Yanga utadhani uwanja ni big deal
 
Simba na yanga wakishindwa kujenga viwanja chini ya hawa wawekezaji mo na Gsm sidhani kama kuna muwekezaji wa ndani atakuja kuweza kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom