Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,353
- 1,234
Juzi nilikuwa kwenye kitchen party ya shoga yangu na mama mmoja aliyekuwa karibu yangu akasema WANAUME WENGI USIWAONE WANAJIDAI BURE, HAWAJUI KUFANYA MAPENZI!! He, nilishtuka kidogo na kutega sikio langu kwa karibu nitapet kusikia zaidi. Baada ya kusikiliza kwa kirefu nikajua kuwa hoja kubwa ya yule mama ni kwamba wanaume wengi hawajui kufanya mapenzi, hawafundishwi jinsi ya kuishi na wanawake kama ambavyo sisi wanawake tunavyofundishwa kwenye kitchen party. wanaume wengi hawana sehemu yoyote zaidi ya vijiweni, majarida na kwenye party., wanawake wanafundishwa jinsi ya ku handle wanaume, kusihi nao, kuwavumilia na mengine. Lakini wanaume hawafundishwi wafanye nini kwenye ndoa zao!!!
Nakapata wazo, kuna haja ya kuintroduce unyago wa aina fulani kwa wanaume? Nini kifanyike kuwafunda wanaume hawa? wajue mwanamke anahitaji nini na wao wafanyaje? je JF pekee inatosha? Lakini mbona wanaume wengi hawasomi????
Nimebaki na labda...... naogopa kuingia kwenye ndoa, haya niliyosikia ni ya kweli?
wana JF mpo?