Ubaya hizi kazi Kuna wengine walidiriki kuhonga kabisa ili wapate kazi, Ila Sasa wanajilaumu bora asiyepata,,, unakuta mtu anatoka home kwake hadi kufika kituo anachotakiwa kufanye kazi ni kilometers 4, hapo hajapewa pesa za usafiri(bodaboda), maji wala chakula, anapigika na jua mchana kutwa hadi jasho linavujia miguuni tena wadada ndo wanatia huruma na hili jua.
Frankly hizi kazi kama mtu uko na Mishe zako za kufanya ukaingiza 5000 - 10,000 ni bora sana kuliko kuhangaika na hizi kazi..
Kuna wadau huku niliko wamevunja mikataba yao na sasa wako na bodaboda zao wanakimbiza mitaani