Kuna hatari inakuja kwenye swala la Kilimo

Kuna hatari inakuja kwenye swala la Kilimo

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Mwaka huu kuna possibility tena ikawa kama mwaka jana mvua kidogo, na Dalili zimeishaanza kuonekana.

TMA wanasema mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara itapata mvua chini ya wastani, hii ni hatari kubwa sana, pamoja na mikoa mingine mingi kuwa ya Kilimo, huwezi ku ignore mikoa hii mitatu kwenye kilimo, Wakulima wa hii mikoa mitatu ni wakulima wakubwa sana ambao production yao huwa ina impact kubwa sana kwenye nchi, Maeneo kama Kitetto au Babati, Hanang, Arusha Dc na Kilimanjaro kule kuna mashamba makubwa balaa, ni kawaida kukuta mkulima kalima hekari 600 mahindi,

Sasa kama kaskazini itakuwa tena kama mwaka jana basi tujiandae tena kwa balaa la pili na huenda likawa baya zaidi kuliko la mwaka huu.

Hata kwenye mifugo tutarajia bei za nyama kuzidi kupanda sana na pia vyakula vya mifugo kupanda ziadi na zaidi kiasi cha watu kushindwa hata kufuga.
 
Huku nilipo mvua wiki ya pili haijanyesha jua kali balaa, mahindi yanakauka
 
mahindi mwaka huu kizungumkuti m nimeshindwa kutia mbolea ya pili shambani kwangu naogpa kupoteza sabaabu hakuna mvua
 
Duu, poleni Sana. Nilikua natamba na jamaa yangu juzi kwamba mwaka huu mazao yatakua tele kwa reference ya mikoa ya nyanda za juu kusini na kati maana huku si alizeti, viazi, mahindi yamesimama hatare na mpaka sasa chini pa bichi mahindi ya kuchoma hukosi baadh ya maeneo.
 
mahindi mwaka huu kizungumkuti m nimeshindwa kutia mbolea ya pili shambani kwangu naogpa kupoteza sabaabu hakuna mvua
Uko wapi!?

Kwa huku mbeya naona hali sio mbaya tutavuna vizuri na mvua bado zipo.. mahindi yanatoboa tunaangaika na mipunga sasa..
 
Back
Top Bottom