Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
KUNA HATUA HUPIGI KWA SABABU KUNA WATU UNAWANG'ANG'ANIA, WAACHE.
Yawezekana ikawa ni kuoa/kuolewa umekuwa kwenye mahusiano na watu ambao kihaiba ni KATAA NDOA na wewe unaona ndio aina/type yako kumbe wanakuchelewesha tu
Sio vibaya kujiuliza kwanini kila mahusiano yako hayazai ndoa? Shida ni wewe au ni aina ya watu unaochagua? Badili aina ya watu.
Yawezekana ikawa ni mafanikio ya kiuchumi hupigi hatua kwa sababu aina ya rafiki ulionao ni ile ambayo wewe unachimba shimo wao wanakuja kufukia usiku ila mchana wanakwambia mpo pamoja .
Sio vibaya kuchunguza marafiki zako na uhusiano wao katika mafanikio yako la sivyo usikubali kuwa na watu ambao wanakuzika huku wakikuaminisha kuwa bado upo hai .
Yawezekana ni mafanikio ya ki elimu umeingia kwenye mfumo wa watu ambao wao wanasema muhimu D MBILI TU 😊 na wakati malengo yako yalikuwa ni kufanya vizuri zaidi ya hapo
USIKUBALI WAKUFANYE URIDHIKE USIPOSTAHILI
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako