kuna hili neno "DAMSHI" sijui limetokea wapi na nini maana yake

kuna hili neno "DAMSHI" sijui limetokea wapi na nini maana yake

Hazchem plate

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
11,048
Reaction score
15,465
Sasa hivi kila kona ukipita utasikia "Damshy" Si makanisani wala Misikitini kote huko utasikia "DAMSHY". Si Wamama wala Wababa kila mtu anasema "DAMSHI"

Hivi hili neno limetoka wapi na maana yake ni nini?????? Maana naona linanikera na huku silielwei
 
Siti ya pili na popcorn yangu....nadamshi tyuuuuuuuu!!!!!
20180826_183455.jpg
 
Sasa hivi kila kona ukipita utasikia "Damshy" Si makanisani wala Misikitini kote huko utasikia "DAMSHY". Si Wamama wala Wababa kila mtu anasema "DAMSHI"

Hivi hili neno limetoka wapi na maana yake ni nini?????? Maana naona linanikera na huku silielwei
Nilijua ni sawa na kudanga. Kumbe sio...

Vijana wana maneno saana. Kiswahili kikue
 
Kudamshi,kushitua, kuchangamsha, kuamusha... kifupi ni kujiongeza kweli hali iliyopo ama uliyonayo.
 
Sasa hivi kila kona ukipita utasikia "Damshy" Si makanisani wala Misikitini kote huko utasikia "DAMSHY". Si Wamama wala Wababa kila mtu anasema "DAMSHI"

Hivi hili neno limetoka wapi na maana yake ni nini?????? Maana naona linanikera na huku silielwei
Maana ya neno kudamshi ni kupendeza au kuendana na mazingira.
Mtu anapokuambia nywele zako zimedamshi ana maana kwamba nywele zako zimekaa poa.
 
Neno Damshi ni msimu ulioibuliwa karibuni ktk jamii na kupewa nguvu zaidi na wasanii wa Bongo fleva (rejea wimbo wa Ivrah - Damshi, nk) likimaanisha kupendeza, kuvutia, kunawiri, kustawi, nk.

Kama kawaida ya misimu (maneno yanayozuka katka jamii) neno damshi litatumika na kuwa maarufu na baada ya muda litapotea na likidumu zaidi litaingizwa kwenye msamiati wa lugha yetu ya Kiswahili na kuwa neno fasaha au sanifu.

NB: Mpka sasa sijaangalia kama lipo kwenye kamusi toka awali au la.
 
Back
Top Bottom