Kuna hoja za kumshitaki Dr. Louis Shika?

Kuna hoja za kumshitaki Dr. Louis Shika?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Huku mitaani kuna mjadala mkubwa sana kuhusu Dr. Louis Shika kuvuruga mnada ule wa Nyumba za Lugumi kama ametenda kosa la jinai ama la! Kuna watu wanadai kuwa Dr. Louis Shika hajafanya kosa lolote lile la jinai na itakuwa ngumu sana kuthibitisha mashitaka juu yake.

Lakini kuna kundi linasema kwamba Dr. Shika wakati wa kushiriki mnada ule alikuwa anaelewa kila kilichokuwa kinachoendelea hivyo anawajibika (Liable) kwa matendo yake aliyokuwa ameyafanya kwenye mnada ule.

Kisheria hili suala la Dr. Shika likoje!!
 
Tusubiri wajuzi wa sheria waje ila atashtakiwa nn wakati kasema 900 itafaa zaidi na sio milioni huku akipigiwa makofi kwani kiswahili ni kigumu

Tuwe wazalendo na lugha yetu
 
Tusubiri wajuzi wa sheria waje ila atashtakiwa nn wakati kasema 900 itafaa zaidi na sio milioni huku akipigiwa makofi kwani kiswahili ni kigumu

Tuwe wazalendo na lugha yetu
Halafu ukitilia maanani kwenye mambo ya kisheria ni mchezo wa kucheza na maneno ama kwa kujenga mantiki au kwa kubomoa hoja za mpinzani wako!!
 
Huyo Dk Shika, kuna watu wanene nyuma yake...

He has a strong backup..

Issue ya Lugumi, ilikuwa inahusisha vyombo vya dola, na dola hiyo hiyo ndio inaaribu huu mchakato. ...

Ila pia nabaki kujiuliza, ni tajir gani anaweza kufanya risk kubwa kama hiyo ya kununua nyumba za Lugumi, kama ajipendi
 
Yote kwa yote jamaa amepata umaarufu ndani ya masaa machache sana!
 
Jamaa hayuko sawa, kwa mujibu wa taarifa zinazotoka, ilibidi kwa sasa awe hospitali badala ya kuwa polisi, nimesoma story yake kwenye gazeti la Mtanzania, hana cha strong backup wala nini, yule ni mtu mwenye matatizo makubwa ya afya ya mwili na akili
 
Huku mitaani kuna mjadala mkubwa sana kuhusu Dr. Louis Shika kuvuruga mnada ule wa Nyumba za Lugumi kama ametenda kosa la jinai ama la! Kuna watu wanadai kuwa Dr. Louis Shika hajafanya kosa lolote lile la jinai na itakuwa ngumu sana kuthibitisha mashitaka juu yake.

Lakini kuna kundi linasema kwamba Dr. Shika wakati wa kushiriki mnada ule alikuwa anaelewa kila kilichokuwa kinachoendelea hivyo anawajibika (Liable) kwa matendo yake aliyokuwa ameyafanya kwenye mnada ule.

Kisheria hili suala la Dr. Shika likoje!!
*R.I.P DR. SHIKA😭*

Dr.Shika alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri lakini bahati mbaya elimu yake haijaweza kusaidia taifa hili achilia mbali kumsaidia yeye binafsi.

Wengi walimchukulia kimzaha tangu alipoonekana kwenye tukio la mnada wa nyumba za Lugumi (mia tisa itapendeza). Makampuni ya kibiashara yalitumia umaarufu wake kama fursa ya matangazo lakini yakamuacha hohehahe asiye hata na mahali rasmi pa kuishi. Aliwahi kuripotiwa na kituo kimoja cha TV kufukuzwa kwenye nyumba aliyokua akiishi huko Tabata baada ya kushindwa kulipia kodi.

Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikimdhihaki na vingine kumuita Kalubandika. Lakini bila shaka vilifanya hivyo pasipo kumjua kiundani *Dr.Shika.*

Ni mzaliwa wa kijiji cha Kalemela wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Majina yake halisi ni Louis Shika Kidola. Yeye na ndugu yake Jeremiah Shika Kidola *(marehemu pia)* walikuwa wanafunzi wenye akili sana na waliofaulu vizuri masomo yao ya sekondari kwa alama za juu na kupata ufadhili wa kusoma udaktari nchini Urusi mwaka 1984 hadi 1991 waliporejea na kuanza kutibu hospitali ya taifa Muhimbili.

Mwaka 1994 Louis Shika alirejea Urusi kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamili katika magonjwa ya kuambukiza (MSc in Infectious Diseases) na udaktari bingwa wa magonjwa ya akili Master of Medicine (Psychiatry). Akiwa huko alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya usambazaji wa kemikali viwandani iitwayo Lancefort Ltd.

Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi, na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.

Inadaiwa shirika la ujasusi la Urusi (KGB) liligundua kwamba akina Shika walipata fedha za kuanzisha kampuni kutoka Marekani kama mkakati wa Marekani kudukua taarifa za Urusi. Kwahiyo baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo walikamatwa. Dr.Shika alitekwa na watu waliodhaniwa kuwa majambazi kupewa mateso makali sana ikiwemo kukatwa vidole.

Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi, Patrick Chokala mwaka 2017 alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba ilibidi kutumia mbinu za "kijasusi" kumnasua Dr.Shika na kumrudisha nchini kwa dharura. Tangu aliporejea alijiingiza kwenye ulevi wa kupindukia kutokana na msongo wa mawazo.

Kwahiyo ukifuatilia historia ya *Marehemu Dr.Shika* utagundua hakuwa "kalubandika" kama ilivyodhaniwa. Ni mtu aliyekua na maono makubwa. Kama si mipango yake kuvurugika huenda angekuwa daktari bingwa na mfanyabiashara mkubwa wa kemikali duniani.

Ni kwamba tu alijikwaa, akadondoka na hakuweza kusimama tena. Serikali ilipaswa kumsaidia kusimama lakini nayo ilimtelekeza. Kwahiyo ameishi maisha ya upweke, masononeko na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

Kampuni aliyoanzisha ya Lancefort Ltd ambayo kwa sasa inamilikiwa na serikali ya Urusi (ilitaifishwa) ina thamani ya $27Bil sawa na TZS 60Trilioni (Bajeti ya nchi kwa miaka miwili).
_
Kwa hiyo Dr.Shika alikuwa anajiita "Bilionea" si kwamba alikuwa anaota. He used to have money. Na hiki ndicho kilichokuwa kinamtesa maana alishindwa kukubaliana na hali yake ya sasa. Hakutaka kuamini kama aliwahi kuwa na pesa.

Kujikwaa na kuanguka ni kawaida katika maisha lakini jambo la msingi ni uwezo wa kusimama tena baada ya kuanguka. Whinston Churchil aliwahi kusema "Success is not final and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
_
Mtu kama huyo hakuwa mtu wa "kumchukulia poa" hata kidogo. Serikali haikutakiwa kumtelekeza. Alipaswa kupewa nafasi nyingine. Either angerudishwa Muhimbili kutibu au angetafutiwa fursa mahali pengine ambapo taifa lingeweza kufaidi ujuzi wake na pia ingekua njia ya kumsaidia kuondokana na msongo wa mawazo na kusahau "mabilioni" yake kule Urusi.

*Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza*

C&P from WhatsApp group.

RIP Dr. Louis Shika.

P
 
Back
Top Bottom