howardlite
JF-Expert Member
- Jul 16, 2016
- 242
- 392
Ndugu Watanzania wenzangu, tunafahamu nguvu ya siasa katika taifa letu.Wapo wenye vyama vya siasa na wapo Watanzania wengi wasio na vyama ambao wote kwa pamoja tumekuwa tukiathiriwa chanya au hasi na matokeo ya uwepo wa siasa kwenye taifa letu kwa kuzingatia kuwa hayo ndio maisha ya kila siku.
Kuna watu watakubaliana na mimi kwenye vyama vya siasa mwaka huu,viongozi na wanachama wanahitaji hekima kubwa,kuvumiliana,kuchukuliana,kupendana na kuwa na busara kubwa kwa kuangalia njia sahihi na muelekeo sahihi wa kufuata.
Kuna watu katikati yenu mwaka huu watakuwa tayari sio kusimama na maslahi ya vyama vyao bali kusimama na maslahi ya taifa kwanza.
Watatokea watu kupinga waziwazi mienendo miovu kwenye vyama vyao ambayo kama aina hiyo ya watu watakuwa madarakani sio vyama vyao tu bali na nchi itakuwa mahali pabaya.
Tazamieni wataibuka watu kupinga rushwa,ufisadi,kuonyesha wao ni wazalendo wa kweli,wapigania maslahi ya ama Tanganyika,ama Zanzibar au Tanzania kwa nguvu na namna hamjawahi kuona,iwe CCM, CHADEMA, ACT nk.
Watu watajiuliza maswali na kuamini wao sio sehemu ya mifumo mibovu na mibaya kwenye vyama vyao na kusema hawa tunawaamini sio kama wale.
Kuna vuguvugu la udini liko chini sana wengine wanajua lakini kadri siku zinavyosogea kuelekea nani wapitishwe kuwa wagombea na wagombea wenza kwenye vyama vyao,hili halitaepukika.
Wenye nafasi za kupitisha majina,kupendekeza nk,msijaribu kupuuza hisia za Watanzania kwenye maeneo nyeti hata kidogo.Kumbukeni kauli za waasisi wa taifa hili.
Sheria na taratibu zenu za kupata viongozi kama mtaruhusu kuwabeba watu fulani kwasababu za fedha,haiba,nasaba au sababu zozote zisizo kuwa sehemu ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo yenu muwe na uhakika mipasuko itakayotokea itawagharimu sana kama chama,mtagharimu umoja na mshikamano wa watu wenu na majeraha yake hayataishia ndani kwenye vyama bali kwa taifa pia.
Mnakumbuka miaka kadhaa Zanzibar?Mnakumbuka nyakati za kuzomeana,ndugu kwa ndugu kuchukiana hakuna kuzikana na uhasama mkubwa?
Watanzania hawa mnaowajua mkiamini siku zote ni wapole kitu ambacho ni kweli,mkiamini hawawezi ku-react na nikama alivyowasema hayati raisi fulani wa nchi jirani zetu,kuna siku inakuja joto ndani ya vyama vyenu litawaamsha na hakuna atakaye amini kama ndio hawa wa Januari 2025.
Mungu ibariki nchi yetu ya Tanzania,wape viongozi wote hofu yako na kuweka mbele maslahi mapana ya nchi na wananchi.
Tuepushe na viongozi wa hila na wasiofaa kwa nyakati kama hizi kwa taifa letu na kutuepusha nao.
Amen