A
Binafsi yalinikuta haya, wiki mbili nyuma. Nilikua nanunua maji dukani kugeuka washafunga gari kwa nyororo!Kwa madereva kwani wamekuwa wakikamata kwa uonevu unakuta dereva kaegesha sehemu ambayo muhusika wa ku-scan anaku-scan ila wao wakipita wanakukamata wakati ushascaniwa. Na pia wanakuta dereva amepark gari kwa dharura kawasha double hazard bado wanakukamata.
Pia wakikukamata wakikupeleka ofisini kwao wanakupa form yenye maelezo ya kulipa faini isiyokuwa na control number ukiwaambia wakupe control number wanakuzungusha wakitaka ulipe pesa cash .
Na pia tunaomba Serikali iingilie kati kiwango cha faini wanayotoza kulingana na aina ya kosa lenyewe kwani faini inayosomeka kwenye form yao ni Tsh 80,000.
Nilikutana na dereva wa pikipiki za gurudumu tatu 'bajaji', hawa wa mtandao, ameingia kituoni akawa anawasiliana na abiria, wakamkamata na kumtoza 80k!Hizi kampuni ni jipu haswaa. Wanazunguka na Bajaj yao, kuwinda watu, kuna siku Nimesimama pia kituoni naongea na simu, mara hao wakanivamia Umefanya wrong parking.
Nikawauza maana ya wrong parking ni nini, na kama naongea na simu nilitakiwa nifanye nini?
Wakajibu ulitakiwa uwashe hazard, nikawauliza hazard kwa sababu gani na why hazard wakati sijamzuia yeyote kupita na nini kazi ya hivi vituo/Flash parking? Na kama mimi wa gari binafsi siruhusiwi kupak Mbona wakala wa barabara hajaniwekea kibao cha no parking?
Nikawauliza so nyie na bajaj yenu hapo mmefanya wrong parking sio Mbona mnanisemesha hapa mmesimamisha hapo Bajaj yenu na hamjawasha hazard?
Kiufupi niliwaka, wakawasha bajaj yao wakatimua kimya kimya!
Walowapa hii contract kwa kweli wajitafakari, wanakera sana na ni wapigaji mnoo