Kuna kaupepo fulani sio kazuri kanapita

Kuna kaupepo fulani sio kazuri kanapita

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Nawasalimu Ndugu zangu.

Kuna ka upepo fulani kanapita hapa nchini. Kwa siku napokea simu hadi 10 zinaomba hela.

Mimi mwenyewe najaribu kutafuta pesa ila imekuwa ngumu. Kila mtu analia na hata Biashara hazijachangamka kabisa.

Kipindi cha sikukuu kama hiki manunuzi yamekuwa ya chini kulinganisha na miaka mingine.

Waziri wa fedha anajua pesa ziko wapi?. Waziri wa Mipango anasema je?

Je, ni kweli kwamba Vikoba vinaondoa pesa kwenye mzunguko na kuwaacha watu na madeni ya kudumu?
 
Ni watu wako tu wamezoea kukupiga vizinga,
Na matumizi ya sikukuu bado hayajaanza, pia miaka hii sikukuu zainakosa mvuto sanaa so usitegemee kuona manunuzi ya juu, watu wataendelea kununua vyakula vya kama siku nyingine tu
 
Nawasalimu Ndugu zangu.

Kuna ka upepo fulani kanapita hapa nchini. Kwa siku napokea simu hadi 10 zinaomba hela.

Mimi mwenyewe najaribu kutafuta pesa ila imekuwa ngumu. Kila mtu analia na hata Biashara hazijachangamka kabisa.

Kipindi cha sikukuu kama hiki manunuzi yamekuwa ya chini kulinganisha na miaka mingine.

Waziri wa fedha najua pesa ziko wapi?. Waziri wa Mipango anasema je?

Je, Nikweli kwamba Vikoba vinaondoa pesa kwenye mzunguko na kuwaacha watu na madeni ya kudumu?
Adui wa mzunguko wa pesa kwa mwezi December ni huu upuuzi wa English medium schools. Watu wanakuwa over sensitive na matumizi ili walipie ada mkuu. Siku hizi hata wauza karanga barabarani watoto wao wanapeleka english medium za kaj...mba nani.
 
Nawasalimu Ndugu zangu.

Kuna ka upepo fulani kanapita hapa nchini. Kwa siku napokea simu hadi 10 zinaomba hela.

Mimi mwenyewe najaribu kutafuta pesa ila imekuwa ngumu. Kila mtu analia na hata Biashara hazijachangamka kabisa.

Kipindi cha sikukuu kama hiki manunuzi yamekuwa ya chini kulinganisha na miaka mingine.

Waziri wa fedha najua pesa ziko wapi?. Waziri wa Mipango anasema je?

Je, Nikweli kwamba Vikoba vinaondoa pesa kwenye mzunguko na kuwaacha watu na madeni ya kudumu?
Yatapita tu komaa.
 
Ngoja tumalize kulamba asali tutawafikiria😁

OIG (7).jpeg
 
Ngoja tumalize kulamba asali tutawafikiria😁

View attachment 2840119
CCM ni watu wabaya sana. Yaani kakikundi ka watu wachache tu, halafu kanakula karibia nusu ya keki yote ya Taifa. This is not fair at all.

Wakati unalia kuhusu ugumu wa maisha na ukosefu wa pesa kwa ujumla mtaani! Wenyewe wanakushangaa!!
 
Back
Top Bottom