Shaksi Msovieti
New Member
- Feb 2, 2025
- 1
- 2
Habari JamiiForums.
Naomba msaada, mimi ni mgeni katika kijiji fulani, wilayani Magu Mkoa wa Mwanza. Katika kijiji hiki kuna utaratibu kwa wageni wanaoingia kuishi kama wapangaji kulipa fedha za kiingilio kiasi cha shilingi elfu 36 ndipo usajiliwe ama ujiunge kama mwananzengo na utambulike kama mkazi rasmi.
Tofauti na hapo, kuna vitisho kwamba unaweza usitambulike au kutishiwa kufukuzwa. Je hii ni sawa.
Tunaomba Mamlaka za Wilaya situsaidie katika hilo maana imekuwa kero na usumbufu sana. Je ni halali kisheria viongozi wa mtaa/kijiji kulipisha watu ili wajiunge kwenye kijiji au mtaa?
Kama ni halali, ile haki ya Mtanzania kuishi mahali popote iko wapi? na je Serikali inatambua huu utaratibu wa baadhi ya maeneo katika wilaya zetu, maana naamini si kila sehemu kuna huu utaratibu.