Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili mwaka huu CCM inatoka madarakani

UKAWA ndio ilikuwa silaha pekee ya kupambana na CCM haya mengine ni ukuda tu. Kilichobaki wapambane tu mwakani waambulie hata ruzuku ya kulambia bia.
 
Washika bunduki!?, Unamaanisha vita au!?, Mkuu nadhani hauko sawa kiakili🤨🤨
 
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kwamba ccm ilishajifia mikononi mwa mzee Kikwete, ndio maana waliweka mtu mpya ambae hakutarajiwa miongoni mwa wale waliokuwa wakitajwa tajwa. Chama kimebaki jina na maamuzi ya mtu mmoja kutegemea na namna atakavyo amka. Ili isionekane kuna migogoro ndani ya chama kwa mtu mmoja kuhodhi mamlaka kamili, wameamua kutengeneza matukio kuzima migogoro halisi isionekane nje ya chama. Ni bahati mbaya sana tulio wengi hatulioni hilo tunafuata mkumbo. Mh Juma Shamhuna katika hafla moja aliyoalikwa aliwahi kusema, namnukulu "sio kila ngoma mtu unatakiwa kuingia na kucheza, kwa sababu ngoma nyingine ni za kichawi". Kwa sanduku la kura ccm ilishakufa, kilichobaki sasa hivi nikuchezeshana ngoma za kichawi tu na yeyote anaweza kutolewa kafara.
 
Mkuu CCM ya sasa ni Strong kushinda CCM yeyote toka mwaka 1977. Sasa ni rasmi CCM imerudi kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Mwenyekiti Magufuli amefanya kazi kubwa sana kurudisha heshima ya chama hiki. Sitegemei kwasasa kama Tanzania kuna chama cha upinzani kinaweza kushika dola.
 
Huu ujinga wenu wa kuwafanya watu waamini ujinga wenu sasa umepitwa na wakati
 
Mkuu, umeandika bandiko refu lenye aina fulani ya ukweli ndani yake, lakini pia unasahau baadhi ya mambo muhimu yanayofanya bandiko likose uaminifu.

Hao wanafiki waliomo CCM ikianguka watakula wapi?
Ungeeleza kuwa kuna maandalizi ya ndani kwa ndani ya CCM ili wanyukane na kumwondoa huyu wasiyemtaka, hapo kidogo ungeonekana kuwa mkweli kidogo.

Lakini utegemee mtu yeyote ndani ya CCM afanye juhudi za kusaidia upinzani ushinde? Hili linatakiwa kujengewa hoja nyingine mbali ya hii uliyoiweka hapa.

Wanafiki wa CCM wataumia humo humo, ndani kwa ndani ili mradi matumbo yao yajae.
 
Kweli wewe upo Tila lila. [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ccm ilikiuka zindiko sababu ya corona mwenge haukukimbizwa ili kupumbaza akili za watz, thus mwamko Ni Mkubwa sana
 

Uliyoyaandika yameanza kudhihirika. CCM ijiandae kukabidhi Ikulu.
 
Wanafiki utawaweza?humu ukanda hasa ileee kaskazi umejaa sana.
 
Katiba katiba katiba, NEC, NEC, NEC
 
Ccm ilikiuka zindiko sababu ya corona mwenge haukukimbizwa ili kupumbaza akili za watz, thus mwamko Ni Mkubwa sana
Kwa hiyo wewe huelewi sababu ya kuzuia mbio za mwenge ni kuepuka misongamano eti?je wewe akili yako pia ilipumbazwa na mwenge?
 

Kichekeso, muono ulio tetereka.
 
NDOTO ZA MCHANA SAA SITA. ENDELEA KUJIFURAHISHA. KWA KAZI ALIYOFANYA JPJM NI WAZI KABISA ATASHINDA KWA KISHINDO. HATA MEDIA ZA ULAYA ZIMETABIRI ATASHINDA KWA ZAIDI YA 80%. ILA NAJUA MTASEMA MMEIBIWA KURA MAANA MNAFIKIRI WATANZANIA HAWANA AKILI YA KUONA UONGO WENU, ETI MIRADI YA UMEME, SGR, BARABARA, NK HAIMWENDELEZI MTU!!!!!!! KWELI??JAMANI TUNA AKILI ZETU HATUDANGANYIKI.
 
Angekuwa amefanya makubwa ungeandika kwa herufi ndogo Ila kwa vile hajafanya kitu unatulazimisha
 
Ata makonda mlisema ivi ivi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…