Zamazangu
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 849
- 497
Katika pitapita yangu nimekuta walimu wa Sekondari halmashauri ya wilaya ya Masasi wakibadilishana mawazo lakini katika hali ya kulalamika kuwa kuna kiongozi mmoja ndani ya idara ya Elimu Sekondari hana utu.
Nilitamani sana kujua ana matatizo gani hasa, yafuatayo yalibainishwa kuwa ndiyo matatizo yake.
1. Anapenda sana rushwa hasa inapotakiwa kulipwa malipo ya kisheria kama vile likizo uhamisho nk yale yanayotolewa ndani halmashauri. Yeye ana tabia ya kuchelewesha malipo ambayo yako tayari na ili ilipwe basi unapaswa kumpigia simu ili muongee, nadhani hapo ninaeleweka, wakati mwingine anaweza kukupigia kukuarifu kuwa kuna malipo yanaandaliwa kwa hiyo jiongeze.
Kwa muktadha huo wapo walimu hasa wale wasiopenda rushwa hawajalipwa madai yao kwa miaka kadhaa wakati wale wanaoona kutoa rushwa sio issue wanalipwa mara nyingi. Uchunguzi ukifanyika itadhihirisha hili ninalolisema.
2. Ana tabia ya kuchelewesha taarifa muhimu zinazohitajiwa kutendewa kazi na kuziomba kwa wahusika nyakati za mwisho, hii husababisha mshike mshike usio na sababu.
Viongozi wa shule na wasaidizi wao huwa na wakati mgumu sana maana utasikia anasema " hakikisha taarifa inafika kwangu by kesho saa 4 asubuhi," tena umebaki wewe tuu wenzako wote washawasilisha. Nk
Mambo haya na mengine mengi yanavunja sana moyo watumishi wa umma. Tufanye kazi kwa kupendana maana sisi sote ni ndugu na tunajenga nyumba moja.
Ahsante