Kuna kitu hakipo sawa kwa media au msanii mwenyewe

Kuna kitu hakipo sawa kwa media au msanii mwenyewe

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
Ndugu wanajamvi nimeusikiliza wimbo wa msanii anajiita ZAIID unaitwa wowowo. Ni msanii mzuri aliyekuja na wimbo mzuri sana lakini cha ajabu hapati promo kwenye media za Tanzania hata kidogo. Nina uhakika huu wimbo wake angeiimba msanii mwingine maarufu basi ungekuwa wimbo wa taifa. Inawezekana menejimenti ya msanii pia haipo vizuri kwenye maswala ya promosheni lakini media pia za Tanzania zinazingua sana.

 
Ngoja nikusaidie jibu: Ni msanii mwenyewe.

[HASHTAG]#upuuzi[/HASHTAG].com
 
Huyo yupo Tamaduni Muziki wenyewe wanasemga wanafanya underground hip hop ambayo haitaji kupingwa redioni maana wenyewe hawafanyi mainstream hip hop.

So kama unataka wa kumpa lawama walaumu wenyewe Tamaduni Muziki na sio Media
 
aisee huu wimbo mkali sn kila nikiinaga wowow mtaani lazima niusikilize huyu Zaiidi anatatizo nishasikia kwny radio nyingi anaitwa kwny interview halafu hatokei au anachelwa kuja
Radio inayopiga huo wimbo sana ni Times fm
 
Sanaa ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine. Unahitahi strategy ili ukupe faida. Kujua kuimba na kuwa na sauti nzuri sio mafanikio ya sanaa ya muziki. Utaishia kusifiwa pasipo kupiga hatua kama huna mbinu za kuupeleka muziki wako mbali.

Namuelewa sana mond kwenye suala la mbinu. Yuko vizuri ndio maana anatusua. Anajua anafanya nini na anataka kiwe nini. Hivyo ndivyo sanaa inataka.

Sio wengine wamebaki kulalamika wakisubiri wabebwe. Kubebwa kwenyewe wanataka wao ndo wafuatwe
 
Naukubali huu wimbo jamaa kautoa wakati muafaka ambapo wenye makinikia ndo wanatamba mjini na bush
 
Hyo ni bonge ya.ngoma mzee, EA radio wanaicheza karibu kila cku lkn

"Hata ujirembe vp Si tunatazama WO WO WOOO"
 
Back
Top Bottom