Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Magazeti ya Guardian la Uingereza na Washington Post la Marekani yamechapisha wiki iliyopita habari za siri kutoka taasisi ya usalama wa taifa CIA.Habari hizo zinaeleza jinsi taasisi hiyo ambayo ni mojawapo ya taasisi muhimu za upelelezi za Marekani ilivyonasa mawasiliano ya simu na kupitia mtandao kwa mfano wa Verizon,Google,Apple na mtandao wa kijamii wa Facebook.Magazeti hayo yalithibitisha uwepo wa nyaraka zinazothibitisha kuwepo mpango wa siri wa ukaguzi kwa jina PRISM .Taarifa hizi inasemekana zimevuja kutokana na mtumishi wa zamani wa CIA Bwana Edward Snowden, kuvujisha siri hizo.
Katika ripoti hiyo; Inadaiwa katika eneo la Africa kusini mwa jangwa la Sahara; Eneo linalochunguzwa zaidi ni Kenya na Kenya ni miongoni mwa nchi ambako mawasiliano ya mtandao yanasikilizwa. Katika ripoti yake ya tarehe 10/06/2013 Yenye Kichwa cha habari "Hati za siri za Marekani zafichuliwa" ; Hamidou Oummilkheir wa DW, anasema "Mashirika ya upelelezi ya Marekani yanapeleleza katika sehemu nyengine pia za dunia.Katika eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara,Kenya imeorodheshwa kama nchi inayokamata nafasi ya mbele kabisa miongoni mwa nchi ambako mawasiliano ya simu na mtandao yananaswa.Kenya imeorodhweshwa katika eneo la rangi ya manjano pamoja na Saud Arabia,Jordan,Ujerumani."
Maswali ninayojiuliza sasa ni;
1.Kenya kuna nini?
(a) Ni nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi hata kuleta mashaka katika nchi nyengine?
(b)Ni mashaka ya uwepo wa kundi la AL-shabaab katika nchi ya Somalia ambayo imeakana na Kenya?
(c)Inawezekana Kenya inatumiwa na baadhi ya nchi kuhujumu miradi na mikakati ya Marekani Africa?
(d)Inawezekana kwa kuwa Kenya ina nguvu zaidi kiuchumi katika soko la Africa Mashariki, basi Marekani wanataka waishike Kenya kwa Remote Control na kwa kufanya Hivyo watakuwa wameishika Afrika ya mashariki nzima?
2.Ikiwa Marekani ina Wasiwasi mkubwa na Kenya kutokana na ujirani na Lilipo kundi la Al-Shabaab la Somalia na hivyo kuhofia kwamba wanaweza kujenga mtandao Kenya; Je! Tanzania tunachukua tahadhari gani kiusalama ukizingatia kwamba Tumepakana na Kenya na tayari kuna fununu kwamba kuna Watu wanaenda somalia na wengine wanatoka huko wanaingia Tanzania kupitia boda ya Mandera(Kenya-Mkoa wa Pwani (Kenya)-Nairobi (Kenya)-Namanga(mpakani)-Longido -Oldonyo sambu(Tanzania)-Ngaramtoni (Tanzania) na Kisha kuelekea wanakotaka?
Nahisi ipo haja na hoja ya kuchukua tahadhari hapa!