Kuna kitu kinafanyika gereza la Ukonga

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Posts
8,546
Reaction score
855
Sijui ni nini lakini kama wkipata facilities naona litakuwa gereza linaloongoza kwakutoa ma grads


Sijui Governor wa lile Gereza ni nani lakini I'm curious kujua what exactly anachokifanya mle tena katika mazingira magumu



Nchi zilizoendelea ukigraduate basi na kifungo kinaondolewa kwani wao wanaamini kuwa Gereza au Jela ni chuo cha kurekebisha tabia ...na hivyo ndivyo ilivyo hata Unguja ambako wao hawana GEREZA bali wana chuo cha kurekebisha tabia

anyway news za huyo mfungwa hizi hapa:

http://issamichuzi.blogspot.com/2009/12/mfungwa-mwingine-ala-nondozzz-gerezani.html#comments
 
Nchi zilizoendelea ukigraduate basi na kifungo kinaondolewa kwani wao wanaamini kuwa Gereza au Jela ni chuo cha kurekebisha tabia ...na hivyo ndivyo ilivyo hata Unguja ambako wao hawana GEREZA bali wana chuo cha kurekebisha tabia
Kwa ufupi ni Chuo Cha Mafunzo
 
..hivi Karume na Kilango nao wamehitimu frm the same univ inayowapa wafungwa wa Tanzania shahada?

..nina mashaka makubwa sana na credibility ya hicho chuo.
 
..hivi Karume na Kilango nao wamehitimu frm the same univ inayowapa wafungwa wa Tanzania shahada?

..nina mashaka makubwa sana na credibility ya hicho chuo.
Umeshaanza...!
 
Kwa jinsi mazingira ya Jela za tanzania yalivyo halafu eti mtu ka graduate???!!! mhhh sijui...
 
Kwa jinsi mazingira ya Jela za tanzania yalivyo halafu eti mtu ka graduate???!!! mhhh sijui...
Mmeshaanza chimbachimba zenu.

Kama mlimsikia vizuri graduate wa juzi alisema kwamba anapata support kubwa sana toka kwa walimu, ikiwa ni vitabu na maelekezo, na alisema kuwa manyampara wamempa chumba cha peke yake ambapo anapata muda mrefu sana wa kuchimba na kufanya assignments!

Anastahili bana!
 
Kwa jinsi mazingira ya Jela za tanzania yalivyo halafu eti mtu ka graduate???!!! mhhh sijui...


Yeah thats means the guys is very intellingent ingawa ameanza hiyo barchelor 2001...nothing else!
 
after all.........it's an open university hence no need of asking many questions because we know the reality.
 
GT uko sahihi kabisa, ni wakati wa serikali na idara ya Magereza kulifanyia kazi jambo hili ili kuongeza idadi ya Grads miongoni mwa wafungwa na kuwa na taifa lenye wasomi na raia wema wengi
 
Mugabe ,Mandela at one time walisoma Open University!Tanzania bado kuna watu wanafikiria UDSM only is a legitimate UNI?
 
..hivi Karume na Kilango nao wamehitimu frm the same univ inayowapa wafungwa wa Tanzania shahada?

..nina mashaka makubwa sana na credibility ya hicho chuo.


Mkuu JokaKuu acha hizo. Kile chuo ni credible and acredited!!! Yaani unanishangaza eti kuwa kule magerezani hakuna wafungwa ambao wana akili?? Kumbuka kule kuna watu wa form six ambao pengine walipata makosa au ya kweli au kusingiziwa kama ilivyo jadi yetu na wakawa pale wakati wana division zao one kali au two unataka wakae huko wasisome??


Kumbuka pia kule magereza kuna maofisa wasomi walifungwa tu kwa sababu ya sheria na wanarekebishwa tabia zao??

Mkuu sasa mimi nitakuwa na wasiwasi na level ya elimu na uelewa wako wa kuchambua mambo!!!!!!! Please, please, think aloud!!! kwa mapana na marefu.

Kwa kuwa tu wachache wanamchukia madame Anne Kilango Malecela, adui wa mafisadi basi mnataka kuona eti chuo not credible?? Hatari hapa!!! Let us be objective!!!!
 
Frankly speaking mtu akimaliza uko yaani huwa naona kama sio graduate vile mniwie radhi kwa ilo.ntajaribu nipate one of the graduate nifanye nae kazi nione kama hisia zangu ni kweli au...........
 
All in all hatakama jamaa angekua kamaliza Diploma kwa mazingira ya magereza amejitahidi sana. wengi tu tunawajua wamesoma with all resources lakini wamediscontinue just in first year, wengine wana swap vyuo kila leo hawajamaliza

Penye jitihada tutoe pongezi
 
Frankly speaking mtu akimaliza uko yaani huwa naona kama sio graduate vile mniwie radhi kwa ilo.ntajaribu nipate one of the graduate nifanye nae kazi nione kama hisia zangu ni kweli au...........
Njowepo wapo magraduate wa celebrated universities na wana deliver nothing, na wapo magraduate vya vijichuo tuu ambavyo vipo vipo, na wanafanya makubwa. Tusiwahukumu wasomi wetu kwa vyuo walivyosomea, bali tuwahukumu kwa wanadeliver nini kwa usomi wao chenye manufaa kwa taifa.
 
Maane,

..watu wa PR ya hicho chuo wana makosa hapa.

..kila mtu anaelewa mazingira magumu yaliyoko kwenye magereza yetu.

..sasa huwezi kukisifia chuo kwa kubobea ktk kuwapa shahada wafungwa.

..binafsi nashauri Idara ya Magereza ingeanzisha chuo chao wenyewe ambapo wafungwa watasoma na ku-graduate huko.

..halafu sasa hivi kuna vyuo vikuu vingi tu. sioni sababu ya watu kama Karume na Kilango kujibanana na wafungwa na walalahoi huko open university. mbona John Magufuli amekaza msuli na kupata PhD toka Mlimani?

NB:

..je, hawa wahitimu wa Open Univ wanaweza kupata admission kwa postgraduate courses ktk vyuo vya kawaida?
 
jamani jiulizeni huyu mfungwa amefungwa lini na shule alianza lini. wengine gereza linawakuta wakiwa shule. chapili nikuwa miaka yote tunalalamika juu ya hali mbaya magerezani, leo watu wanapewa hali zao za msingi wengine mnafikia kusema mna mashaka na vyuo walivyosoma. mimi ninawasiwasi na elimu ya hawa wenye wasiwasi na OUT pasipokuwa na sababu za msingi. kama wewe ni daktari wa binadamu lazima ujue huwezi kuwa sawa na mwanasheria. aidha usijigambe unafahamu zidi ya mwanasheria.
jiulizeni, miaka yote munaona jinsi mahabusu wanapopelekwa mahakamani walivyokuwa wamechafuka. juzi si mmeona babu seya na wanae walivyopendeza??? mnataka kusema babu seya ana jera ya pekee??? . hayo ni mabadiliko yanayotekea magerezani, ambayo ni matokea ya kukua kwa haki za binadamu.


gereza chuo cha mafunzo, mtu akigraduate afutiwe atolewe gerezani!. hilo sio kweli, hakuna nchi iliyoendelea inafanya hivyo!!!, yawezekana akahamishiwa kifungo cha nje, lakini si kuachiwa huru kwa kigezo cha elimu. chuo cha mafunzo zanibar unafunzwa juu ya kile ulicho kosa , na si kila jambo. mathalani ulivunja myumba ukaiba. upo gerezani umesomea ualimu, kifungo hakiwezi katishwa kwa kuwa una degree ya ualimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…