Wapinzani ni kama manabii, wabashiri na watabili na huwa wanachokisema kinatokea, mimi nawaona kama ni watu muhimu sana kiroho hawa wapinzani wa Tanzania. Wakatia wa awamu ya nne ya Mzee Jakaya wapinzani walisema mengi tena waziwazi majukwaani. Mfano huyu ni Rais dhaifu, nchi hii inahitaji Rais mbabe, na kweli tukampata. Nani anabisha.
Wakasema tunataka Rais atakaekuwa anakusanya kodi, kweli akaja na tumejionea, nani atabisha? ajifanye kama ananyoosha kidole tu.
Wakasema tunataka Rais atakae kuwa haangalii sura ya fisadi kweli akatokea, na wote tumeshuhudia kwa macho watu wameumia na wengine wametoroka nchini.
Jamani watabiri hawakukaa kimya sasa hivi wanataka Rais atakaye lokudouni nchi kwa ajili ya Korona, wenyewe tumeona kipaumbele chao hatakufikia hatua ya kijilokudouni wenyewe. Hivyo utabiri hapa ni watu kufungiwa ndani mpaka hapo korona itakapoisha kama mwaka mwaka au wazungu watakaposema basi. Na mimi naona kama mambo tayari yapo jikoni kwani sasa wanaachiwa haya mambo watalaamu wa elimu ya kizungu ya utabibu ndiyo wenye maamuzi ya mwisho ambao hata dawa bado hawajagundua hao wazungu. Utabiri wao unatimia suni.
Kuhusu kufufua shirika la ndege na elimu bule haya wanakili walikosea kuyaingiza katika utabiri. Nawashauri watanzania tuungani na wapinzani kwani Mungu anawasikiliza sana na tabiri zao zinatokea tena akyuresi kabisa.
Mimi mtoto wa Mchungaji na maliza kwa kukumbusha maneno yanaumba, na likiumbika tusibadilishe gia angani.