kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Mimi ni mshabiki wa Yanga tena kindaki ndaki kabisa, lakini matokeo haya nimeyapenda maana yametupa somo fulani.
Jana nilivyokuwa naangalia jinsi timu yangu na wale Waarabu wa mchongo wanavyocheza (nina maana Al Hilal), nikaona Yanga tuna timu ila hatuna uzoefu na mashindano haya.
Ukiangalia vizuri Waarabu wale wa mchongo walivyokuwa wanacheza, walikuwa hawana papara. Walicheza mpira wa kutulia baada ya kupata goli, hawazingatia kutafuta goli la pili bali walilinda goli lao kuanzia kwenye dakika ya 4 mpaka mwisho wa mchez,o walicheza kwa kutulia sana.
Naamini na sisi tumejifunza kitu kupitia wao, yale mambo yetu sijui watapigwa kama ngoma tuachane nayo. Yale ndiyo yaliweka wachezaji wetu presha ya bure, naamini tukitulia tutafika mbali kwenye michezo ya CAF Federation.