Kuna kitu nimejifunza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Mimi ni mshabiki wa Yanga tena kindaki ndaki kabisa, lakini matokeo haya nimeyapenda maana yametupa somo fulani.

Jana nilivyokuwa naangalia jinsi timu yangu na wale Waarabu wa mchongo wanavyocheza (nina maana Al Hilal), nikaona Yanga tuna timu ila hatuna uzoefu na mashindano haya.

Ukiangalia vizuri Waarabu wale wa mchongo walivyokuwa wanacheza, walikuwa hawana papara. Walicheza mpira wa kutulia baada ya kupata goli, hawazingatia kutafuta goli la pili bali walilinda goli lao kuanzia kwenye dakika ya 4 mpaka mwisho wa mchez,o walicheza kwa kutulia sana.

Naamini na sisi tumejifunza kitu kupitia wao, yale mambo yetu sijui watapigwa kama ngoma tuachane nayo. Yale ndiyo yaliweka wachezaji wetu presha ya bure, naamini tukitulia tutafika mbali kwenye michezo ya CAF Federation.
 
Siku hizi Kuna tofauti kubwa sana kati ya manager na head coach.. sasa yanga wanamfanya Nabi kama manager.. he is responsible with everything.. yeye ndo anaamua yanga ishinde au isishinde[emoji23].. hii ni hatari, ndo maana wazungu wakaanza kutumia director of football na technical directors kufacilitate kazi za manager na manager kubaki kama head coach.. Sasa siku nabi kaamka vibaya yanga haishindi.. [emoji23] ni hatari sana hii.. mwinyi zahera anaitwa mkurugenzi wa ufundi ila sijui aliishia wapi.. angetusaidia sana.
 
Mngejifunza kwa Simba pia..mbona nao wamecheza hivyo
 
Nyie wenzenu wanaweka kambi nje ya nchi wanacheza na kina TP mazembe na kina Asante kotoko nyie mnajifungia kigamboni mnacheza na Afrika lyon kwa ufupi viongozi wa Yanga hawana akili

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
Halafu wachambuzi maandazi wakawa wanaiponda Simba kwakuweka kambi nje ya Nchi, nakuisifia yanga kuwa wapo sawa, gssm anatembeza bahasha kwa wachambuzi maandazi wanaigharimu timu kwa sifa za kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…