A
Anonymous
Guest
Wamekuwa wakitufanyia fujo, wakiona sehemu ipo wazi wao wanavamia wanachukua maeneo hayo kwa nguvu.
Wameshakamatwa mara kadhaa lakini baada ya muda wanatoka, wakipelekwa Polisi huko ndio hawakai kabisa, wakitoka wanawarejea wale waliowashtaki.
Wakikuona wewe ndio una kiherehere wanakwambia kabisa “watakupoteza”. Mmoja wa kiongozi wao anaitwa Shabani Mapete.
Viongozi mbalimbali wanajua akiwemo Mkuu wa Wilaya na hivi ninavyoandika hapa kuna kesi inayoendelea Mahakamani kuhusu masuala ya Ardhi, lakini wao hawajali kuhusu kesi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alifika hadi maeneo yetu akaagiza Jeshi la Polisi lifuayilie malalamiko yetu na ikiwezekana matapeli hao wakamatwe.
Wakikamatwa wanapelekwa Kituo cha Polisi cha Chanika baada ya muda wanarejea Mtaani, inawezekana kituo hicho nacho kina shida.
Mapema wiki hii wamevamia shamba la mama mmoja wa hapa mtaani wakaanza kung’oa mazao yake aliyokuwa amepanda, mama huyo hana shida na kesi inayoendelea lakini jamaa wamefika na kuharibu kila kitu, alikuwa anawarekodi lakini hawakujali chochote wanasema wao hakuna wanayemuogopa Serikalini.
Tunaomba ujumbe huu ufike kwa Waziri wa Ardhi, Waziri Mkuu na Rais Samia kuwa kuna Watu huku Pugu wanadai wao hawaogopi Serikali na hawajali maamuzi ya Polisi wala Mahakama, tusaidie tunaishi kwa hofu kama vile Serikali haipo.