Kuna madhara gani gari likikaa miezi sita bila kutumika?

Kuna madhara gani gari likikaa miezi sita bila kutumika?

mediaman

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2011
Posts
451
Reaction score
688
Wakuu, naomba kujua iwapo gari langu nililolipaki mahala karibia miezi sita sasa litakuwa na shida siku nikianza kuliendesha tena.
 
Gari halina tatizo lolote.

KM sio mtaalam mwite fundi akuwashie.

KM unaweza anza kucheck km Oil ipo level. maji kwenye rejeta na betri km ni nzima tairi upepo upo! washa ondoka
 
Halitakuwa na shida Mkuu ila zingatia yafuatayo:
Battery itakuwa imeisha chaji bila shaka, kwa hiyo itahitaji boosting. Terminal zake pia uzicheki.

Matairi yatakuwa yameisha upepo na hivyo utahitaji kuyajaza upepo au kuyaweka mapya.

Tank litakuwa limeanza kupata kutu. Liangalie kwa umakini.

Kama kuna panya, bila shaka baadhi ya nyaya zitakuwa zimekatika au kuchubuliwa. Ziangalie.

Badili oil. Iweke nyingine mpya.

Litakuwa chafu mno. Hivyo lioshe kwa sabuni na kulipaka mafuta ya kondoo 😂😂😂

Kila la kheri. Bila shaka balance ya mafuta hujaisahau bado.
 
Kwanini uweke miezi sita bila kulitumia?

Nahisi battery itakufa. So angalau kama wewe una safiri muachie mtu funguo hata awe analiwasha kwa dakika 10 linaunguruma hafu analizima.

Ila angekua analitembeza hata dakika 10-20 mara moja kwa week 2-3 itakua salama zaidi.

Kumbuka: Gari sehemu kubwa ni vyuma, sasa vyuma vikikaa vimezubaa mahala ambapo vipakutana na unyevu na hewa ya oksijen vinaweza tengeneza kutu (sio kila mahala, zile sehemu ambazo hazina rangi wala rust-protection), sasa assume zile sehemu ambazo zinazunguka/suguana zikapata kutu, itasababisha ugonjwa.
 
Wakuu, naomba kujua iwapo gari langu nililolipaki mahala karibia miezi sita sasa litakuwa na shida siku nikianza kuliendesha tena.
Hapo nenda garage wataalamu wa hayo mambo wapate chochote
 
Madhara ya gari kutotumika ni makubwa kuliko kutumika. Kumbuka gari limetengenezwa ili litumike na si vinginevyo
Usipolitumia siku ukiliamsha utalitengeneza kwa gharama kubwa zaidi
 
Mkuu unafanana sana na mwanangu mmoja Daktari wa meno

Pia anafanya kazi tanesco
 
Wakuu, naomba kujua iwapo gari langu nililolipaki mahala karibia miezi sita sasa litakuwa na shida siku nikianza kuliendesha tena.
Showroom kuna magari yanakaa zaidi ya mwaka na ikifika siku linauzwa vizuri tu.
Angalia tu panya wasiingie,chomoa betri tu
 
Hapo kwa muda huo utahitaji betri kwa ajili ya kucharge,
 
Showroom kuna magari yanakaa zaidi ya mwaka na ikifika siku linauzwa vizuri tu.
Angalia tu panya wasiingie,chomoa betri tu
Huwa wanayatoa wanayazungusha na kuyawasha kila baada ya muda fulani. Haujawahi kwenda showroom ukakuta gari zimetolewa na kuanza kupangwa upya.
 
Madhara yapo aise kama hukutumia gari kwa muda mrefu.

Mfano mdogi tu mwezi uliopita nilikuwa na shughuli za mikoani kwa mwezi mmoja na wiki moja.
Gari niliacha nimeipaki uani ambapo jua na mvua kama kawaida.

Ase imenibidi baadhi ya tabia za gari zinifikishe gereji.
 
Huwa wanayatoa wanayazungusha na kuyawasha kila baada ya muda fulani. Haujawahi kwenda showroom ukakuta gari zimetolewa na kuanza kupangwa upya.
Sio kila showroom wanaweza kufanya hivyo, ila gari inaweza kukaa muda mrefu bila madhara iwapo umeipaki sehemu nzuri.
 
Back
Top Bottom