Kuna madhara ya kupunguza mbuzi pembe?

Kuna madhara ya kupunguza mbuzi pembe?

dudupori

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
1,795
Reaction score
1,914
Habari wadau, nimeanza kamradi ka ufugaji wa mbuzi hivi karibuni ila tatizo kuna baadhi ya mbuzi pembe zao zina ncha kali hivyo naona kama zinahatarisha wao kwa wao kuumizana, nimepata wazo la kuwapunguza pembe hivyo naomba ushauri ikiwa kutakua na madhara kwani umri wao ni zaidi ya mwaka mmoja...
 
Kuna mbuzi amewahi kuleta mashitaka kwako kuwa kajeruhiwa na mwenzake?

Kama hakuna acha kuwapunguza.
Hapa unahitajika ushauri wa kitaalam na sio mipasho, wafugaji walio wengi hupunguza pembe wangali bado wadogo kuepusha hizo athari hasa kwa wale wanaofugwa na kulishwa ndani ya banda...
 
Nimefuga mbuzi najua nachosema. Wanyama wanajua namna ya kuishi siyo kama wewe ukiwa na panga mkononi basi kila mtu akukimbie.

Kuna mtu huwa anakata nyati pembe?
 
Nashukuru pia kwa kuchangia, kuna tofauti kubwa kati ya kuwa mfugaji na kuishi na mifugo hivyo ingekua vyema zaidi nipate ushauri toka kwa wafugaji wabobezi na sio wewe unayeishi na mifugo, nadhani tumeelewana usipende dandia mada usizozijua...
 
Sasa mbona wewe unaishi na mifugo ina maana ABC kuhusu mifugo umekuja kuzijulia huku.

Wakate na miguu kabisa.
 
Kiuhalisia kama Pembe zetatolewa vyema hakuna madhara yeyote yatakayomfika mbuzi husika. Ila kama zitakatiwa chini sana karibu na fuvu basi kuna hatari ya kuweka wazi sehemu ya ubongo na hatua stahiki zisipofanywa basi mbuzi/kondoo/Ng’ombe atapata madhara.

Faida moja wapo ya kutoa pembe ni Kupunguza hatari ya kujeruhi/kuumiza wanyama wengine na ayamtunza. Rahisi kudhibitiwa.

Kwa Maelezo zaidi
Wasiliana na Sipy Vet Centre kituo cha huduma za mifugo. +255764667 503
 
Shukrani kwa ushauri mkuu...
 
Sasa mbona wewe unaishi na mifugo ina maana ABC kuhusu mifugo umekuja kuzijulia huku.

Wakate na miguu kabisa.
Mbona unaleta ubishi usio na faida?
Mbuzi kitaalamu kama pembe zinakua kubwa ni vyema kuzijata hasa kwa mbuzi wa kisasa ili kuepusha hatari za kuumizana wao kwa wao au hata wewe mfugaji!
Sio mbuzi tu hata ng'ombe tunakata pembe na nguruwe vile vile tunakata meno kuzuia hilo la kuumizana!

Nakubaliana na mdau hapo juu wewe umeishi na mbuzi hujawahi kufuga mbuzi!
 
Leo niko ibadani. Subiri kesho.
 
Hakuna madhara...kikubwa hakikisha unazikata bila kutikisa ubongo asije pata kichaa...akawehuka.
 
mkuu unaweza punguza mbuzi pembe ila nakushauri ita mtaalamu wa mifugo. mbuzi anaweza kukatwa pembe zile zilizochongoka na kufanywa butu ili zipunguze madhara si wao kwa wao tu pia kwa wale wawahudumia(hasa kwa wale wa maziwa wafugwao ndani).
ILA mbuzi si maranyingi sana kuumizana
 
Mbona unaleta ubishi usio na faida?
Mbuzi kitaalamu kama pembe zinakua kubwa ni vyema kuzijata hasa kwa mbuzi wa kisasa ili kuepusha hatari za kuumizana wao kwa wao au hata wewe mfugaji!
Sio mbuzi tu hata ng'ombe tunakata pembe na nguruwe vile vile tunakata meno kuzuia hilo la kuumizana!

Nakubaliana na mdau hapo juu wewe umeishi na mbuzi hujawahi kufuga mbuzi!
Huyo mbwiga msamehe bure kila kitu anajifanya mjuaji wakati anaishi na mifugo...
 
mkuu unaweza punguza mbuzi pembe ila nakushauri ita mtaalamu wa mifugo. mbuzi anaweza kukatwa pembe zile zilizochongoka na kufanywa butu ili zipunguze madhara si wao kwa wao tu pia kwa wale wawahudumia(hasa kwa wale wa maziwa wafugwao ndani).
ILA mbuzi si maranyingi sana kuumizana
Nimekupata vyema kiongozi....
 
Back
Top Bottom