Uchaguzi 2020 Kuna mahali CCM ilikosea?

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Wakuu heshima sana,

Kadri siku ya uchaguzi mkuu zinapokaribia nabaki najiuliza maswali kadhaa bila majibu.

Najaribu kutafakari ni eneo gani haswa CCM ilikosea ?.

Mosi, kununua wapinzani (wabunge, madiwani na viongozi wa vyama).Wananchi au ukipenda unaweza kuwaita wapiga kura hawapendi siasa za aina hiyo.

Ukinunua wabunge au madiwani yawezekana bado haujanunua wapiga kura au sababu za kuchagua upinzani bado zinakuwa pale pale !.

Pili, Style ya kutawala au kuongoza za utawala huu si rafiki au wapiga kura hawazipendi.Hivi siasa za kutumbua tumbua fukuza fukuza mara vyeti feki bado si jawabu la kupendwa ? !.Labda tuseme kulikuwa na uonevu,kukiuka sheria na taratibu za ajira au vyote kwa pamoja.

Tatu, Matumizi ya kupiliza ya vyombo vya habari kusifiwa na majivuno. TBC chini ya Dr Ryoba ilipitiliza kusifu kila jambo mara ndege, Reli, Vyeti feki lakini Makonda hahusiki na ukaguzi. Barabara hata ya Kilometer 2 mtu atasifiwa kuanzia asubuhi hadi jioni kuanzia Jumatatu hadi Jumatatu nyingine ni mwendo wa kumsifu mtu mmoja ungefikiri kujenga Daraja au Kivuko ni hisani kumbe ni wajibu wake tena kazi yenyewe kaiomba kwa kampeni na ahadi luluki.

Nne, Unasema pekee yako miaka mitano wengine wakisema shida (Kesi, Vifungo, misukosuko....) Nauliza WaTanzania wamechoka na siasa za aina hii !.

Tano, Ujenzi wa Flyover Dar una faida zipi kwa mkaazi wa Dongobesh au Tarakea mkulima wa ndizi au mkulima wa Ngogwe Lushoto.Naamini kila eneo la nchi yetu lina mahitaji yake ya msingi kutokana na mazingira yake.

Sita, Watawala wetu walifika mahali wakajiona hapo walipo walifika wenyewe si wananchi /wapiga kura. Kauli zao maamuzi yao mengi yalilenga kuwanufaisha wao wenyewe eg kupitisha sheria za kuwajengea nyumba MaRais wastaafu. Sheria za mafao yao na matibabu yao zipo vizuri kweli kweli wakati wafanyakazi sheria za mafao yao kila mara wanatengenezewa sheria za kuwakandamiza eg sheria ya kujitoa na kikokoteo. Sheria za kinga ya kutoshitakiwa hata wakifanya makosa ya aina gani !.

Mwisho nadhani watawala hawakujiandaa kukumbana na uchaguzi wenye ushindani wa kiwango hiki tunachokiona sasa. Walifikiri kumnunua Silinde, Lijualikali, Nassari ...... watakuwa wamemaliza kila kitu sasa wamekutana na uungwaji mkono wa kiwango cha kutisha kutoka kwa mgombea wa CHADEMA.

Tangu mfumo wa siasa wa vyama vingi kuanzishwa tumewaona wagombea walioleta kashi kashi za kutisha.Mwaka huu 2020 tumeanza kuona dalili mbaya kwa baadhi ya mikoa ambayo chaguzi za nyuma walikuwa wakiunga mkono CCM. Mkoa ya Rukwa, Katavi, Simiyu, Ruvuma, Lindi na Mtwara ni ngome ya CCM kwa muda mrefu lakini tumeshuhudia katika uchaguzi huu wananchi wa mikoa hiyo wakibadilika na hivyo kuiweka CCM katika wakati mgumu.
 
Wabunge wote wapuuzi tuu hasa wale wa kijani kibichi... Wanatunga sheria ya mafao mpaka miaka 60 halafu wao kila baada ya miaka 5 wana chukua chao.

NI UONEVU WA HALI YA JUU SANA. PIA 15% YA HESLB NI UKATILI WA HALI YA JUU SANA TENA BILA ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA MIAKA 5.
 
Dawa hapa ilikuwa kumhonga mwananchi was kawaida, sii kumhonga kwa maana ya rushes laa, Ila kumpatia mahitaji yake ya muhimu, kulingana na mazingira yake, huduma ya afya, maji, huduma wezeshi kwa mkulima, mazingira rafiki ya biashara, mazingira rafiki ya usafiri kulingana na maeneo.

Na sii kumrubuni mwanasiasa kwa maana ya kuwahadaa wafuasi wake juu ya kukubalika au kutokubakika kwa chama.
 
Kutegemea dola badala ya hoja, wameitumia police kuuwa upinzani imeback fire polisi wamechangia kuimarika kwa upinzani Hadi vijijini.
Lolote baya walilowatendea watz limerudi kwao mara 7.
.wamebandika mabango nchi nzima.
.wamezuia media zote
.wametumia wasanii wote
. wanatumia police
. wametumia time
.wametumia msajili
Lkn vyoote vimebuma.
Chama mfu Ni kile kinachobebwa na dola badala ya nguvu ya umma. Anaemiliki nguvu ya umma ndie anaemiliki dola.
 
Ebu taja kila eneo ambalo unafikiri walikosea.

Mosi,Gwajima kugombea ubunge Kawe.
Mkuu serikali ya Magufuli imekuwa na mapungufu mengi ambayo wananchi tumeona ni usanii tu tunahubiriwa ni mpenda haki lakin kuna wala rushwa ambao yeye mwenyewe kawasema wakina Lugola.
Ila hawajachukuliwa hatua yeyote wakati wengine wakibambikiwa makosa yasiokuwa yao.

Lakini pia imekuwa kawaida kwa CCM kugeuza nchi kama ni yakwao peke yao. Hii imeleta utengano na vyama vingine kuona wanaonewa na kiongozi ambae wengine walimpigia kura japokuwa sio ccm.
 
Ccm na vyama vilivyoiasisi wamekaa madarakani kwa miaka 51+ lakini wameshindwa kuitoa nchi kwenye umaskini wa kila kitu!

Yaani imekosa hoja za kuwashawishi wananchi na badala Yake wanawalazimisha wananchi wawakubali kwa majigambo ya kipuuzi kabisa!

Kujitapa kuwa wamejenga barabara, while, zahanati na miradi ya maji hiyo siyo hisani kwani ni wajibu wa serikali ambayo inakusanywa Kodi kutoka kwa wananchi! Hili ndio kosa kubwa wanalolifanya ccm!

Kujificha kwenye issue ya amani kila wakati as if tuna ugomvi na majirani nalo ni kosa la kiufundi wanalofanya na litawapunguzia Sana wapiga kura!

Wanasahau kuwa mwl. Nyerere alishalimaliza hili kwa kuukataa ukabila Somo ambalo lilieleweka kuliko masomo mengine kwa wananchi! CCM wameuvaa ukanda na ukabila pamoja na udini vitu ambavyo ni simu kwa umoja na utengamano wetu Kama taifa! Sasa wanashindwa kuyaunganisha makundi haya waliyoyasisi wenyewe na yatawasumbua mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…