Uchaguzi 2020 Kuna mahali CCM ilikosea?

Wachache watakuelewa kiufupi Chadema wali outsmart CCM,kutumia ushawishi wa mataifa ya magharibi.
Bwana yule aliamini hakuna upinzani, aliamini anaungwa mkono na kila mtz, bara na visiwani na mpaka ulimwengu mzima, wali underestimate, otherwise wangalijua hali ingekuwa hivi, hakika TL, wangemzuia asije nchini, wangetumia mbinu zote, zilizo chini ya jua, abakie huko huko.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kama kuikataa CCM ni unafiki itabidi baraza la kiswahili wabadili maana ya neno unafiki.
CCM yangu ( yetu ) ina Wapiga Kura wake Milioni 22 'Kitakwimu' na 'Kiutafiti' hadi leo hii sasa Wewe 'Kisokolokwinyo' Mmoja tu una 'Athari' gani?
 
Mazingira magumu kwa wafanyabiashara Miaka hii 5 imekuwa ni balaa kwa mfanyabisahara mkubwa na mdogo. Kila mmoja anaogopa hata kuweka pesa benki wakihofia zitakwapuliwa na TRA.

Mheshimiwa ametuambia yeye hataki mambo ya kupangiwa yeye ni rais anayejiamini. Kwahio ni moja kwa moja kwamba ametuacha nje wananchi yeye anafanya anayoyafikiria yeye!
 
 
CCM yangu ( yetu ) ina Wapiga Kura wake Milioni 22 'Kitakwimu' na 'Kiutafiti' hadi leo hii sasa Wewe 'Kisokolokwinyo' Mmoja tu una 'Athari' gani?

Endelea kuamini takwimu za Polepole,CCM haina wanachama 1 million.

WanaCCM asili wanajua hali halisi ilivyo sasa huko site.

Polepole muumini wa serekali 3 na Dr Bashiru CUF damu hawakijui chama asilani hawa ni wageni baada ya uchaguzi watatimuliwa bila kuzingatia matokeo ya uchaguzi.

Hawa wamemdhalilisha Mwenyekiti,wamemfikisha mahali pagumu hadi kufikia kupiga magoti loh salaleeh watatimuliwa mapemaaa.
 
Jmn tukapige kuraaa#Oct.28 delete CCM,tuandike historia mpya.

Kichinjio changu leo nimekitazama na nikakiweka mahali salama hadi 28/10/2020 kitafanya yake 🐐
 
Hivi kadi ccm ya Bashiru ni namba ngapi ?
 
CCM walijikoroga walipomuajiri Polepole na digirii yake ya unafiki
Sasa unawaweka benchi akina Januari Makamba kwa kuwafitinisha na Mwenyekiti
Miamba ya Siasa kama kina Kinana ndio wangeiweza kasi ya Lissu sio haka ka Chawi ambako kamezeheshwa na roho mbaya ya Kichawi
Polepole ni bure kabisa ni Butu kisiasa na kijamii
 
Probably, lkn shida ilitokea hivi:-
(i). Kwenye vyeti feki - hapa ilitakiwa waachishwe utumishi ila mafao yao wapewe (Michango yao pspf, gpf, nssf);

(ii). Kwenye kutumbua - ilijenga visasi kwa watumbuliwa mfano kwa wakati mmoja awamu ya kwanza aliwaweka pembeni DED takriban 125, DAS takriban 80, RAS takriban 21, DC takriban 73 nk nk. Hali hiyo ilidumu;

(iii). Mishahara hewa - hapa napo hakushauriwa vizuri sababu Serikali imeendelea kubeba mzigo wa ilipaji mishahara ambapo wale wote waliotumbuliwa wameendelea kulipwa mishahara ya viongozi ilihali wakiwa benchi - so, nafasi moja kama ya DED unakuta inalipiwa mishahara miwili au mitatu (mmoja wa DED aliyepo na mwingine wa DED aliyetumbuliwa);

(iv). Lugha za majukwaani: - issues za tetemeko kagera (maneno yanafahamika), wakati akiwa Magu halafu wananchi wakamwambia kuwa wana njaa (maneno aliyojibu), nk nk

Hayo na mengine mengi uanatuongezea mzigo kuyasafisha ila - mitano tena kama mtahiari sawa
 

Umesema vema mkuu.
Watanzania kiasili ni watu wanaopenda HAKI na kuishi kwa UPENDO kati yao.
MIAKA HII 5 MAGUFULI AMEVUNJA SANA HAKI ZA WATU NA KUWEKA DOUBLE STANDARDS KIASI KWAMBA WATU WENGINE ESP. CCM NA WATU WANAOMSIFU WAO WAKO JUU YA SHERIA. HILI LIMEWAKWAZA SANA WATANZANIA WENGI IKIWEMO WANA-CCM.
VILEVILE KUPENDA MISIFA YA KIJINGA KWA KUTAKA KILA KITU ASIFIWE YEYE HATA SHULE IKIJENGA CHOO PIA VIMEFANYA WATANZANIA KUMKINAI MAGUFULI NA KUONA NI MBINAFSI NA ANAJIKWEZA.

HATUTAKI TENA RAIS WA NAMNA HIYO.

NDIO MAANA TUMEMKATAA PAMOJA NA "MAZURI" ALIYOYAFANYA.
 
Magufuli anataka kuendesha chama kama jeshi la mtu mmoja.

Watu wengi wamemuachia chama.

Serikalini kashasema hapangiwi kitu.

Washauri wanamwambia anachotaka kusikia tu.

Kwa mfumo huo, si ajabu akipoteza ushawishi, ukiindoa kondoo wake ambao watamfuata hata akiwapeleka machinjioni.
 
Hivi kadi ccm ya Bashiru ni namba ngapi ?
Namba milioni 21,laki3, elfu67, mia9 na 85
21,367, 985...
Slow Slow kasema wapo wanaCCM hai mil22. Huyu alikuwa CUF kindakindaki ni muhamiaji!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Fikra chakavu za mwenyekiti,na unafiki wa wana ccm ndiyo umetufikisha hapa...
 
Ni butu kwerikweri....
 

Mbona kama kuna dalili zote CCM kwishey
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…