Kuna maisha halisi ya mtaani na ya mtandaoni, tunakuja mitandaoni kujipooza tu, Mtandaoni hakuna masikini, usiyumbishwe

Kuna maisha halisi ya mtaani na ya mtandaoni, tunakuja mitandaoni kujipooza tu, Mtandaoni hakuna masikini, usiyumbishwe

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Inabidi sasa tukubaliane na uhalisia, kwa sababu ndio ukweli uliopo sasa hivi ya kwamba tunaishi katika kizazi ambacho watu wana maisha ya aina 2.

Kuna maisha halisi ya mtaani na maisha ya mtandaoni.

- Unaweza kuwa mtu wa kawaida sana mtaani ila huku mitandaoni unaheshimika
- Unaweza kuwa huna marafiki wengi mtaani, ila huku mitandaoni una followers 100k
- Unaweza ukawa umesota sana huku kitaa, ila mitandaoni unatusua

Ubaya ni kwamba maisha ya mtandaoni hayalipi bills. Unaweza kuwa influential huku mtandaoni, ila mwisho wa mwezi landlord anataka hela yake, hajui maswala ya kuwa ww unaheshimika ukiwa online.

Asubuhi/jioni vituo vya dalala watu wamejaa kinoma wanagombania usafiri, watu wanapigana vipepsi, ila ukija mitandaoni kila mtu ana gari. Vijana wengi wanasurvive kwa sababu wazazi wao ama ndugu bado wanafanya kazi, hiyo ndo pona pona. Wapo watu wanakula na kulala kwao, akiotea laki 1 kwa mwezi ndio hiyo siku atapiga fujo vby mno mitandaoni

Point yangu ni - tumia mitandao kwa machale sana. Kila mtu anapitia kipindi kigumu, kila mtu ana shida zake, kila mtu anasota kwa namna yake... ground spana zinatembea kwa kila mtu, usidhani ni ww tu ndo huna bahati, huku mtaani watu tunashikishwa ukuta na life tunakuja mitandaoni kujipooza. Usiyumbishwe na kelele za mitandaoni. Ignore the noise, follow the signal.

BE YOU,
DO YOU,
FOR YOU

Source : Sir J instagram
 
Mitandaoni kila mtu mambo yako juu ya rula, tena wanaoandika “hasubui badala ya asubuhi, hacha badala ya acha wana shida sana!!!
 
Tuko kimatrix matrix vile hatujui ni uhalisia wa maisha inawezekana kile kitu ni ndoto tu hakuna uhalisia.
 
Umeandika ukweli kabisa ila kwakua hawakusumbui wala hawaleti mazara yoyote kwako acha waendelee na maigizo.
 
Eti landlord anataka hela yake hajui suala la wewe kuheshimika ukiwa on line😀

Mkuu si mbaya kujifariji lkn😀
 
Mitandaoni kila mtu mambo yako juu ya rula, tena wanaoandika “hasubui badala ya asubuhi, hacha badala ya acha wana shida sana!!!
Ukiona mtu ana matamshi ya hivyo jua ni muhaya
 
Inabidi sasa tukubaliane na uhalisia, kwa sababu ndio ukweli uliopo sasa hivi ya kwamba tunaishi katika kizazi ambacho watu wana maisha ya aina 2.

Kuna maisha halisi ya mtaani na maisha ya mtandaoni.

-Unaweza kuwa mtu wa kawaida sana mtaani ila huku mitandaoni unaheshimika
-Unaweza kuwa huna marafiki wengi mtaani, ila huku mitandaoni una followers 100k
-Unaweza ukawa umesota sana huku kitaa, ila mitandaoni unatusua

Ubaya ni kwamba maisha ya mtandaoni hayalipi bills. Unaweza kuwa influential huku mtandaoni, ila mwisho wa mwezi landlord anataka hela yake, hajui maswala ya kuwa ww unaheshimika ukiwa online.

Asubuhi/jioni vituo vya dalala watu wamejaa kinoma wanagombania usafiri, watu wanapigana vipepsi, ila ukija mitandaoni kila mtu ana gari. Vijana wengi wanasurvive kwa sababu wazazi wao ama ndugu bado wanafanya kazi, hiyo ndo pona pona. Wapo watu wanakula na kulala kwao, akiotea laki 1 kwa mwezi ndio hiyo siku atapiga fujo vby mno mitandaoni

Point yangu ni - tumia mitandao kwa machale sana. Kila mtu anapitia kipindi kigumu, kila mtu ana shida zake, kila mtu anasota kwa namna yake... ground spana zinatembea kwa kila mtu, usidhani ni ww tu ndo huna bahati, huku mtaani watu tunashikishwa ukuta na life tunakuja mitandaoni kujipooza. Usiyumbishwe na kelele za mitandaoni. Ignore the noise, follow the signal.

BE YOU,
DO YOU,
FOR YOU

Source : Sir J instagram
Ahahahahahaha! Pia kila mtu ni mbobezi wa masuala ya uchumi, siasa na ujasusi kitaifa na kimataifa. hata kama kitaani anajulikana ni form four leaver!
 
Wanafunzi wa chuo wanafujo sana boom likitoka.
Waacheni vijana ndio wakati wao huu.
Baadaye ngumu kupata nafasi ya kufanya hivyo. Kila kukicha majukumu na mahitaji yanaongezeka.
 
Motivation speaker
Motivation speaker
Motivation speaker
Motivation speaker
 
Na wiki mbili za mwisho inakuaje ?
Kwa wanafunzi wa UDSM wakazi wa Mabibo Hostel wanapiga 'Shuttle Pori" na "kupiga pasi ndefu" kwenye milo.

NOTE:
Shuttle Pori = Kutembea kwa miguu sababu ya kukosa nauli ya shuttle bus,
Pasi Ndefu = Kuruka milo mingine (unakunywa chai na kusubiri mlo wa usiku uki-skip mlo wa mchana, au unaruka breakfast na lunch unapiga mlo wa usiku tu)
 
Back
Top Bottom