Kuna makundi 2 ya watu duniani. Wewe uko kundi lipi?

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
KATIKA MAKUNDI HAYA MAKUBWA MAWILI YA WATU DUNIANI, WEWE UKO UPANDE UPI?!

Na Mikael Aweda.

Duniani kuna aina mbili za watu. Wazalishaji na watumiaji wa kilichozalishwa. Wachezaji na washangiliaji. Wanaofikiri na wanaofikiriwa. Wabunifu na wanaotumia ubunifu wa wengine. Wauzaji na wanunuzi.
Wasemaji na wasikilizaji.

Kwa bahati mbaya, upande wa pili wa watumiaji, washangiliaji, wasikilizaji, wapokeaji, wanaofikiriwa na wanunuzi wa mazao yaliyotoka kwa upande wa kwanza siyo upande mzuri.

Siku zote anayeanza kuzalisha anafaidika na anachowapa wenzake. Mpokeaji analazimika kulipia chochote anachohudumiwa na mhudumu wake.

Matokeo yake ni kuwa mshangiliaji anamtajirisha mchezaji. Mtumia bidhaa anamfaidisha aliyebuni bidhaa. Aliyeajiriwa anamtajirisha mwenye kampuni nk nk nk.

Je, wewe uko upande gani wa pande hizo mbili? Kumbuka ukija duniani na kuondoka bila kuhama upande kutoka upande wa wapokeaji kwenda upande wa watoaji walau kwa cho chote uwe na uhakika kuwa dunia haitakukumbuka kwa cho chote.

Hata ukifa tutalia kwa sababu ya kuwahurumia watoto wako lakini hatutaku--miss hata kidogo kwa sababu hukuwahi kutufanyia chochote cha kukumbuka wewe.

Hata mama Ntilie aka Mama-Lishe na muuza chapati akifa watoto wa majirani zake watasema 'eeeh jamani, mama muuza chapati tamu ametuacha!' Watalia. Wewe utaliliwa na nani?

Mwajiri atajaza nafasi yako baada ya wiki moja. Siyo sababu ya kukumbukwa. Kibao chenye jina lako kitakusemea walau kwa miezi kadhaa baada ya msiba lakini mwisho wako ni baada ya kibao chenye jina lako kuangushwa na mchwa makaburini.

Picha zako unazotupia Facebook kila siku inatusaidia nini? Badili upande. HAMIA AIR MAENDELEO siyo badala ya kurundika akaundi mia za magrupu luluki ya social media.

Andika jina lako vizuri. Vinginevyo, niwe mkweli. Hakuna atakayejua kuwa kuna mtu alikuwepo hapa duniani, kwa sababu hakuwahi kutoa cho chote bali ulikuwa mpokeaji tu tena asiye na shukrani.

Tafadhali, tukutane kesho 17.05.2020 saa mbili asubuhi Tbcfm 90.0 (DSM) Tuendeleze mjadala huu kwa upana zaidi.

Mikael Aweda
078458330
Fb Mikael Aweda
 
Michael habari za siku nyingi sana, ulitoweka jukwaani kwa kitambo mno. Karibu
 
Waambie na waliokomalia mambo ya siasa huku wako palepale hawasogei.
 
Umenena vyema kadri Mungu alivyo kukadiria. Ndugu zangu tunapo zungumza swala la successful people ni jambo ambalo Muumba wa mbingu na ardhi ametupangia tayari.. kila mtu anaridhiki yake.

Lakini hata hivyo lazima dunia iwe na msawazo sawia yaani ecosystems, wote tukiwa wazalishaji nani atatumia bidhaa za mwenzake...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…