Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Kuna vitu vinashangaza sana, wizara ya afya inashangaza sana. Wote tumeshuhudia duniani kote suala la chanjo likiwa mjadala mkubwa sana ambapo kila aina ya utaalam unatumika kwa wanaokubali na wanaoipinga.
Hivyo si suala la kisiasa wala propaganda bali ni la kisanyansi, ndio maana niliona hata hapa kwetu wataalamu wa afya na madaktari bingwa wakialikwa kutolea ufafanuzi.
Ghafla bin vuu anaibuka mtu anaitwa Steve Nyerere eti anapewa ubalozi wa kuhaamasisha chanjo. Steve anajua nini kuhusu chanjo?
Akipigwa maswali mawili tu hataweza kujibu chochote kile kutokana na kutokua na elimu yoyote achilia mbali elimu ya afya ya binadamu, lakini Leo eti nae ni balozi.
Inashangaza na kusikitisha wizara kuandaa kampeni ya kutoa elimu ya chanjo alafu mtu Kama Steve nyerere anakua speaker. Nae anatoa elimu, sitaki kuamini hatuna wataalamu wa kutosha.
Waziri gwajima kuwa serious kwenye hili suala, kumbuka suala la kuhaamasisha masuala ya kitaalamu yanapaswe yaende kitaalamu maana Kuna watu wana maswali yao magumu na yasipojibiwa kitaalamu yatawafanya wakatae.