Kuna mambo tuache siasa, Steve Nyerere hafai kuwa balozi wa chanjo

Kwenye kila jambo utani utani lazima nao uwepo...
Steve Nyerere yuko kwenye utani utani...
 
Hapa hebu tutulie kidogo. Ukisema hivi, unamaanisha jamii ipi hiyo ambayo Steve hawezi kuihudumia? Ni nani huyo wa kumuuliza hayo maswali mawili? Kama Profesa tu anakunywa dawa isiyothibitishwa kitaalamu kwa lengo tu la kughilibu uma, halafu baadae tunaambiwa ile kitu alikunywa ni sampuli,inafanyiwa uchunguzi mpaka leo jii. Au unazungumzia nchi hiihii ambapo wataalamu wa tiba walijenga mtambo wa kujifukiza mahospitalini kwa nia ya kutibu Covid na leo hii wanahamasisha chanjo? Kama haitoshi, unaongelea raia ambao wanaamini kiongozi wao aliweza kuondoa Corona kimiujiza tu? Unaongelea jamii ambayo si prof, si la saba na wala si PhD wanaamini kikombe cha marehemu Ambilikile (Babu) ni tiba ya magonjwa sugu?

Kama unazungumzia jamii hiyo hapo juu, hakika waziri kumchagua Steve Nyerere kunaakisi jamii yetu, yani ni perfect match. Itashangaza sana kumpata balozi umtakae kwa watu type hiyo hapo juu.

Sema Amen!

Hallelujah!
 
Mnahamasisha nini? Acheni ugonjwa ujihamasishe wenyewe jamani, hivi kuna mtu ataona watu wanaugua na wengine wanafariki kwa Corona halafu asiemde kuchanjwa?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…