Habari wakuu,
Husika na kichwa cha habari,
Kama kuna jambo ambalo lilikuwa likiniwazisha ni namna ya kumjua Nabii wa uongo na wa kweli.
Nilisikia habari hizi kutoka katika mahubiri kanisani tokea nilipokuwa mdogo.
Kifupi habari hizi ziliniitisha maana sikuwa najua ya kuwajua Manabii.
Nikakua bado nilisikia tu niendelea kusikia habari za kuja Manabii wa uongo.
Mpaka sasa bado nazisikia habari hizi za Manabii wa uongo.
Watu wanasema Manabii wa uongo tu, je hakuna Nabii wa kweli?
Kama yupo ni yupi?
Wamemjuaje huyo Nabii ni wa kweli?
Biblia inasema neno 1Yohana 4:1
Wapenzi msiamini Kila roho, bali zijaribuni hizo roho, bali ziketoka kwa Mungu
Mathayo 7:15
Jihadharini na Manabii wa uongo, watu wanaowajiq wamevaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu
Mwl Mwakujonga Rabbon
UKIONA YAFUATAYO JUA NI DALILI LA NABII WA UONGO AU KANISA LA UONGO
1. Kanisa lolote/mchungaji anayehubiri kwamba tunahesabiwa haki kwa sheria, sio neema.
2. mtumishi yeyote ambaye ili kumuona unatoa pesa,
3. yeyote anayeoza mafuta ya upako, chumvi,maji n.k
4. yeyote anayeitisha nywele za utosi, kucha au kuosha miguu
5. yeyote anayetangaza kukomboa ardhi,kukomboa pesa,nyumba au mwili kwa sadaka
6. yeyote anayeamini unatakiwa kukomboa laana iliyoko maishani mwako wakati tunajua Yesu Kristo alibeba laana zetu pale msalabani hivyo ukimwamini anakukomboa toka kwenye laana zote, unakuwa mali yake kiumbe kipya kabisa.
7. mtumishi anayependa kujitukuza kama yule wa Kisongo Arusha.
8. mtumishi mwenye wapambe kama yule wa kimara temboni, malawi na masalia yake hapa tz. wapambe yaani mtumishi akiongea kuna kuwa na lijamaa fulani limeshika kipaza sauti linapambisha pambisha yale anayosema mtumishi. wanajaribu kuhamasisha kwa njia ya mwili kumbe maneno yeyote yenye Roho Mtakatifu hayahitaji nguvu ya mwili kuhamasisha au kuleta badiliko.
9. nabii yeyote anayetabiri mabaya tu na anasema tuombe na bado yanatokea. kama waganga wa kienyeji wanaweza kutabiri mabaya, au wakatabiri ukoo wako, au majina yako kama kale kajamaa kahaya branch ya nabii wa malawi tapeli wa south africa na wengine wa uingereza, just to mention a few.
10. wachungaji majority ambao ni masharobaro (though sio wote), ni matapeli. kwanza anapeda kuva vizuriii, gari za garamaaa, analindwa na mabodigadiiiii, ana kiburiii cha pesa...wote hao ni wa ibilisi.
11. wachungaji wote ambao ukimsikiliza akiomba, haamuru kwa JIna la Yesu, ila kwa mamlaka yake yeye mwenyewe, kama yule wa arusha, na wengine.
12. mchungaji yeyote anayepinga na kukosoa Biblia, kama yule wa Arusha na mzee wa neema. wanajiita wakristo ila wanaamin Biblia ina mapungufu, still bado wanaitumia na katika maombi yao hawatumii Jina la Yesu ila mamlaka yao binafsi.watajitahidi hawatataja JIna hilo manake linawaumiza.
13. makanisa yote ambayo hayahamasishi kumtafuta na kumpata Roho Mtakatifu awe kiongozi wako, hilo limepoa na sio kanisa la Kimungu. Roho Mtakatifu lazima umtafute ajae, kwani ndiye atakiusaidia kwenye maombi, kwenye uongozi n akutambua mabaya hata yale yasiyoandikwa kwenye Biblia, pia ni moto ulao akiwa ndani yako ni kwamba Mungu yupo ndani yako hivyo shetani hatakusogelea kirahisi. (labda umruhusu wewe mwenyewe). makanisa ya katoliki, sabato, lutheran (wasio wanafeloshipu au uamsho), mashahidi wa jehova na wengine woote wasio na mfumo wa ujazo wa Roho Mtakatifu, hao sio wa Mungu, kimbia.
14. makanisa yote yanayoruhusu unywaji wa pombe kama katoliki na mengine, wale wenye wachungaji walevi kama mzee wa bapa, kimbia.
wengine ngoja niachie wenzangu.