Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Salaam Wakuu,
Kuna baadhi ya Mawaziri wamekuwa wanang'aa sana kwenye vyombo vya habari na kusifika wa kufanya kazi nzuri katika wizara zao lakini majimboni kwao hali ni mbaya sana. Miundombinu mibovu na matatizo ya msingi kwenye maeneo yao hawayafanyii kazi.
Hapa najiuliza Uwaziri umekuwa mzigo mzito sana kiasi cha wao kushindwa kutimiza majukumu ya majimboni kwao au la. Binafsi ni mkazi wa Jimbo la Ukonga. Mbunge wetu anatamba sana kwenye Wizara yake kwa sasa lakini maeneo ya huku kwetu hali ni mbaya sana barabara hazipitiki. Mbunge wetu hakai nasisi tunamuona tu anatamba na uwaziri.
Binafsi naona ipo haja tutenganishe Ubunge na Uwaziri ili tuwatendee haki Wananchi wanaomchagua kiongozi kuwawakilisha na kuwatetea.
Nawasilisha