Kuna Mazingira ya upigaji na matumizi ya nguvu katika mchakato wa uchukuaji wa aridhi na ulipaji wa fidia Chongoleani Tanga

Kuna Mazingira ya upigaji na matumizi ya nguvu katika mchakato wa uchukuaji wa aridhi na ulipaji wa fidia Chongoleani Tanga

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Kuna maeneo mengi Serikali imekuwa ikitekeleza miradi lakini uenda sio jambo la kushangaza kuwakuta wananchi wengi wanaozunguka maeneo ya miradi husika wananungunika au wanashindwa kuithamini wazi wazi na kuwa waangalizi au mabalozi wa miradi hiyo haswa kutokana na maslahi yao kutozingatiwa ipavyo wakati wa michakato ya kupisha uwekezaji.

Jambo hilo utokana na mambo mbalimbali ikiwemo baadhi ya wananchi kudhurumiwa haki zao wakati wa mchakato mzima wa kuwahamisha wakazi husika kwa lengo la kupisha miradi.

Suala hilo linatajwa kuonekana kujitojeza katika mradi wa Bomba la mafuta Kata ya Chongoleani Wilayani Tanga ambapo inajengwa gati kwa ajili ya kupokea malighafi hiyo kutokea Hoima Uganda.
IMG_20240616_214259_826.jpg

Ambapo kuna madai ya uwepo wa mchezo mchafu unatajwa kuchezwa na baadhi ya mamlaka ikiwemo Halmashauri husika hali ambayo imepelekea baadhi ya wananchi kubakia na manunguniko ambayo huko mbeleni ndio yamekuwa yakiibua hisia za kukosa uzalendo kwenye rasilimali za umma, hususani kwenye miradi ya kimkakati ambayo uanzishwa na Serikali pamoja na wawekezaji mbalimbali.

Taarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali zinaeleza kwamba wananchi walio wengi wamelipwa fidia ya Tsh. Milioni 2 kwenye kila eneo la ekari moja huku wakidai kuwepo kwa mazingira ya kushinikizwa kusaini kutokana na kutiwa hofu .

Chanzo XXX kinaeleza kuwa wengi walishinikizwa kusaini na ambao walionesha kukataa kutia saini kwa kudai kuwa kiasi ni kidogo bado hawakulipwa kabisa badala yake sasa wamejengewa mazingira ya hofu yanayowanyima haki ya kutoa malalamiko yao.

Mzee mmoja wa makamo ambaye ni mkazi wa eneo hilo la Chongoleani ambaye anajishughulisha na shughuli za kilimo na uvuvi anaeleza kwamba kuna utaratibu ambao ulifanyika lakini wanafikiri kulikuwepo na upigaji na udhulumu wa haki katika utaratibu huo.

"Tumeachia maeneo yetu lakini tuliumia, awali tulipata taarifa kuwa mwekezaji alitaka wananchi walipwe pesa nzuri ili kupisha mradi na pesa ambayo ilikuwa ikitajwa ni zaidi ya milioni 15 kwa kila eneo la ekari moja ambapo alilenga kupata eneo la ekari 70, kilichokuja kutokea hao watu wa Halmashauri na mamlaka nyingine walitumia pesa hiyo hiyo na kuitawanya kununua ekari 300, kilichokuja kutokea ni uonevu"alieleza Mzee huyo

Anaendelea "Tunajua vitu vingi lakini watu tumefungwa mdomo kuzungumza, tuliamua kuchukua hizo milioni mbili maana mambo ya Serikali huwezi kuwa na sauti sana hata ukikataa kama wenzetu hakuna namna kama wamepanga eneo kulichukua wanalichukua, lakini kilichotokea sio haki uenda hata mwekezaji mwenye mradi anajua tumepewa pesa aliyoilenga"
IMG-20240612-WA0005.jpg

Katika kufuatilia kwa kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo kwa Mzee huyo inaelezwa kuwa wananchi ambao walitoa eneo la ekari 70 kati ya 300 zilizochukuliwa wamekuwa wakipewa huduma ya vyakula kila Mwezi na fungu la pesa zaidi ya laki 150,000/=, lakini kuna madai kwamba wengine maslahi hayo hayawafikii.

Suala hilo linaendelea kuibua minongono ambapo baadhi wananchi wamekuwa wakijiuliza maswali bila majawabu, kwamba kwanini kumekuwepo na tabaka, ambapo wengine wanapewa huduma hizo za chakula na posho kwa kipindi kadhaa na wengine hawapati .

Hisia hizo zinawafanya kuamini kuwa ekari nyingine zilichukuliwa nje ya utaratibu kusudiwa uliowasilishwa kwa mwekezaji na wahusika hawakuzingatia thamani halisi badala yake kwenye jamii hiyo kumeendelea kuwepo na madai kwamba eneo la zaidi ya ekari 200 zilichukuliwa kwa lengo tofauti na Halmashauri, mamlaka nyingine au watu binafsi wenye maslahi ili kwa mbeleni wapate hela zaidi ikitokea amejitokeza mwekezaji atakayehitaji sehemu ya ekari hizo.
images - 2024-06-16T213440.862.jpeg


Kumbukumbu zinaonesha nini?

Suala hili sio geni mbele ya vyombo vya habari japo limekuwa likiibua hisia tofauti, ambapo baadhi ya wananchi maeneo mbalimbali unapopita mradi huo wamedai kulipwa fidia ndogo ikilinganishwa na thamani maeneo walioachia kupisha mradi, ambapo baadhi yao wamenukuliwa wakisema kuwa pesa haziwawezeshi kupata maeneo mengine kwenye maeneo ya karibu na walipopisha mradi jambo ambalo wadai limeendelea kuwaumiza vichwa na kubakia njiapanda.

May 25, 2024 chombo cha habari cha 'The Chanzo' kilichapisha makala yenye uchambuzi iliyobebwa na kichwa kinachosomeka. "Wananchi Hanang Watishiwa Kupewa Kesi ya Uhujumu Uchumi Wakidaiwa Kupinga Mradi wa EACOP. Wasisitiza Hawapingi Mradi"
Screenshot_20240616-173313_1.jpg

Katika makala hiyo, wananchi wanadai kuwa suala la kudai fidia stahiki kwao imegeuka kaa la moto, hata hivyo baadhi ya wadau kutoka baadhi ya Asasi za Kiraia ikiwemo GreenFaith wamekuwa wakinyoshea kidole mradi huo kuwa umeghubikwa na mazingira ya ukiukwaji wa haki za binadamu hususani kwenye suala la ulipaji wa fidia.

Ambapo baadhi yao wamewa kutoa madai kwa nyakati tofauti kwamba kutokana na kukosoa baadhi ya vitu kwenye mradi huo ujikuta katika mazingira ya hofu kutokana wanachoamini kuwa ni kuhusishwa kwao na mazingira ya hujuma kwenye mradi huo jambo mbalo wanalipinga vikali kwa kusema kwamba dhamira yao ni kusimamia haki na ukweli.

Hata hivyo baadhi ya mamlaka za Serikali zimezikika zikieleza kuwa katika mradi huo mambo yalienda shwari kanagaubaga, hayo yalielezwa Mkurugenzi wa TPDC, Musa Makame Mei 30, 2024 ambapo alinukuliwa akisema kuwa hakuna taratibu zilizokiukwa na kuwataka wasioridhika na fidia hiyo kufuata taratibu za kufikisha malalamiko yao.
IMG_20240616_214259_392.jpg

Lakini pia wananchi hao wanadai kuwa mazingira ya kuwasilisha malalamiko sio rafiki kama inavyoelezwa badala yake wamekuwa na hofu ya kueleza mbele ya umma hata kufikisha madai yao mbele ya vyombo vya Sheria.

Baadhi wananchi wanatoa wito kwa mamlaka za juu, wadau wa Haki za Binadamu, vyombo vya habari kufuatilia suala hilo, huku rai yao nyingine ni kuzisihi mamlaka kuzingatia maslahi ya wananchi inapotokea wananchi wanaachia maeneo kupisha uwekezaji, wanadai kuwa kwa kufanya hivyo itaongeza uzalendo kwa wananchi kuizungumzia vyema miradi mbalimbali tofauti na pale inapotokea haki zao zinapokandamizwa hususani kutopewa maslahi stahiki kupisha maeneo.
images - 2024-06-16T213304.672.jpeg

Tukumbuke ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP),unatekezwa kwa ukaribu zaidi na Kampuni ya TotalEnergy ukitajwa kukamilika mwaka 2025 huku fidia ya kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ilitajwa na mamlaka ya Mkoa wa Tanga kuwa tayari ilitolewa kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom