Kuna mengi nyuma ya pazia kuhusu mkataba wa LUGUMI Enterprises na Polisi

Kuna mengi nyuma ya pazia kuhusu mkataba wa LUGUMI Enterprises na Polisi

M_kara

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2016
Posts
385
Reaction score
293
Baada ya Meneja msaaidizi wa Infosys kutokea kwenye video iliyokuwa akikanusha kuhusika kwa kampuni hiyo na Lugumu Enterprises, mimi niliamua kuwatafuta ofisini watu wa Bio-Metrica LLC, ambao ofisi yao iko Florida nchini marekani.

Katika website yao wameonyesha baadhi ya kazi kubwa walizo wahi kuzifanya. Kilicho nigusa ni baada ya kuona kwamba kazi zao zinazo onyeshwa ni za miaka ya karibuni sana (2014/16). Kwa hiyo nikatamani kujua ni lini kampuni hiyo ilisajiriwa kuanza biashara.

Ikumbukwe kwamba meneja wa Infosys alisema walipewa kazi ya kitaalamu na Bio- Metrica LLC somewhere around October 2011.

Kwanza, niliwapigia simu kwenye namba inayo onyeshwa kwenye website yao, na baada ya kujitambulisha kwa jina nikaambiwa niache namba yangu ya simu (USA) na kwamba wangenipigia muda si mrefu.

Baada ya kusubri muda mrefu, nilipiga tena na kuacha ujumbe mfupi kwenye voice mail yao kuwakumbusha kile walichoniahidi. Kana kwamba hiyo haikutosha, niliwaandikia email nikitaka kujua muda wa uzoefu wao katika shughuli zao.

Hilo nalo halijajibiwa mpaka leo. Kwa tabia za kibiashara za marekani hicho siyo kitu cha kawaida.

Watu wana mtazamo wa kibiashara na kwa hiyo, fursa yoyote inayojitokeza mtu kutafuta taarifa za biashara yako ni kitu kinacho changamkia mara moja.

Hii inaonyesha wazi kwamba yapo mengi nyuma ya pazia. Tender ya ku-supply electronic finger printing identification system nchi nzima ni kazi kubwa, ambayo naamini wangeweza kuionyesha katika website yao kama walivyo onyesha kazi zingine ndogo ndogo.

Na kuna uwezekano kwamba kampuni hiyo pengine hata ilikuwa haijasajiriwa hiyo miaka ya 2011.
 
Mkuu tufunulie hilo pazia basi tuyaone hayo yaliyojificha huko nyuma.
 
Mafuguli kaamua kuwa mpole kwenye hii ishu.

Amepima kina cha Maji, akaona asije zama buree ...
 
Back
Top Bottom