Kuna mgogoro baina ya Okrah na Simba? Viongozi wa Simba semeni ukweli

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Winga Mghana Okrah haonekani dimbani, sijamuona Dubai akiwa benchi wala mchezo wa Leo na Mbeya City ambao tumenusurika.

Hivi hizi tetesi kuwa hana furaha kuchezea Simba na ameomba arudi kwao ni za kweli au vipi kama hataki kuchezea Simba kwanini wamng'ang'anie sasa, wachezaji wa Ghana inaonekana wasumbufu sana nikitolea mfano Morrison, jana kule Singida nao wamemtema kiaina Enock Atta.

Viongozi wa Simba watueleze Okrah ana shida gani, mnapoficha mambo ndipo mnapotupa ghadhabu.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
OKRA ANA MATATIZO YA NIDHAMU, KUJIONA, USHINDANI WA NAMBA NK.

1. Baadhi ya Wachezaji Wengi wa Ghana wamekuwa na MATATIZO ya nidhamu.
Abarola,Lamine moro, Morison nk.

2. Kutokana na ushindani mkubwa Wa Namba Kikosini Simba simuoni Okrah akicheza.
Anachangamoto ya.....

1. Moses PHIRI.
2. Clotus Chama.
3 .Said Ntibazonkiza.
4 .Pape Sackho.
5. Banda.
6. KIBU.
7. Mwinuke.

Katika hili kundi Unatakiwa uanze na wachezaji 2- 3. Tu.
 
Augustine Okrah aliomba kuondoka dirisha hili baada ya namba kuwa ngumu ila uongozi ukaweka ngumu ndio kisanga kimeanzia hapo
 
alimfitini dejan sasa aone fitina zake
 
Sio kila kitu ni cha kuweka hadharani mambo mengine yanamalizwa ndani ya nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…