Kuna mtu anajua mfumo huu

Mtoto Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2014
Posts
300
Reaction score
173
Wakuu,

Idea yenyewe ni hivi, kukopesha wahitaji wa pesa ndogo ndogo watumishi wa uma kwa riba ya 10% kwa mwezi, mfano mtu anakuja unampa laki1, cash then wewe unasubiri mwisho wa mwezi unachukua laki na 10.

Swali ni hivi je ni taratibu gani mtu anatakiwa afanye ili pesa yake ikatwe kutoka kwenye mshahara wake na kwenda kwenye akaunti yako moja kwa moja?

Natanguliza shukrani
 
Hapo Ni ngumu sana maana Wewe sio taasisi ya fedha kisheria, pia makubaliano yako na unayemkopesha hayapitii Kwa mwajiri wa mdeni wako. So simply impossible!!!!
 
inawezekana, kama ukiongea na mwajiri wao, kwa waajiriwa wa sekta binafsi ni rahisi maana , unaweza wewe ukawa unachukua kwa mwajiri wao au mwajiri wao kuwakata na kuweka kwenye account yako. zungumza na mwajiri wao , wao wakubali na mwajiri wao akubali.
 
kumbuka usiseme umemkopesha kwa riba, sema umemkopesha 110 000, ukikosea anakuruka kwani haujasajiriwa, pia hulipii mapato hivyo na ww ujakuwa na kimbembe chako cha kujibu
 
Mtoto Tajiri

usikopeshe watu kwa riba ni haramu. acha mfumo huo. kuna njia zaidi ya bilioni za kutafuta fedha kihalali pitia hapa jukwaani utaziona. Muogope ALLAAH.

"Allaah Amehalalisha biashara na kuiharamisha riba" - (Quran 2: 275)

"Enyi Mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni yaliyobakia katika riba, ikiwa mmeamini. Na kama hamtafanya hivyo, basi fahamuni mtakuwa mmetangaza vita na Allaah na Mtume Wake" - (Quran 2: 278 – 279)
 
Last edited by a moderator:

Basi ngoja nibadili Lugha;Ni hv nataka nikopeshe watu kwa faida
 
kumbuka usiseme umemkopesha kwa riba, sema umemkopesha 110 000, ukikosea anakuruka kwani haujasajiriwa, pia hulipii mapato hivyo na ww ujakuwa na kimbembe chako cha kujibu

Well Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…