Kuna mtu yeyote aliyefungua website ya tcu na aka login

Ni mdogo wangu alichelewa kuchagua udom. Vyuo yake ni
1,st john 2,mihayo<amucta>
3,makumira
4,teku<mbeya>
5,jordan
mbka sasa 4 vimemtema bdo st john.
Ushauri.!
 
Hata sielewi nayo ina majanga gani..kila siku inazingua CAS haifunguki sijui kwa nn
 
Mwambie aanze kufanya maandalizi chuo atapata
 
Education anaweza akapata ila asitegemee sn,kwaa akiba angeomba na diploma kama akikosa tcu akapige dip.
 
Ipo siku nitajifunga mabomu niwatilie timu..au nakwenda kummwagia mtu maji ya pilipili ajue nimembabua na tindikali..
 
Kinachozingua zaidi, kwanini baadhi ya vyuo vinatangaza majina wao hawatangazi ikiwa mchakato mzima wa kuwapata wanafunzi wanaufanya wao, amaizing kiukweli!!!
 
Wadau wa tcu kama mpo humu mtuambie mmefikia wapi cz tupo kama yatima hatujui mnafanya nn na mmefikia wapi na kwanini vyuo vinatangaza wanafunzi na nyinyi kama tume yenye dhamana mpo kimya adi sasa ivi.
 
Ni mdogo wangu alichelewa kuchagua udom. Vyuo yake ni
1,st john 2,mihayo<amucta>
3,makumira
4,teku<mbeya>
5,jordan
mbka sasa 4 vimemtema bdo st john.
Ushauri.!
hata TEKU amekosa??lakini jina lake si halipo kwa watu waliokosa?
 
Vijana kuweni na subira taratibu za TCU ziko wazi kabisa kwamba baada ya kufanya selection awamu ya kwanza na ya pili basibmajina ya wote waliochaguliwa yalirejeshwa katika vyuo husika ili yakaguliwe kabla ya kuwekwa rasmi mtandaoni, hata hivyo baadhi ya vyuo husika vimeamua kujiridhisha na tayari yamewekwa katika website zao mfano: Jordan, Arch'Mihayo, Arusha univerty, Tumaini Makumira, etc. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za kiutendaji tarehe 25August2013, majina yalirudishwa tena TCU ambapo hapo sasa kikao cha pamoja kikaitishwa ili kuyajadili, na wskati hilo linaendelea ndipo nafasi nyingine ikatolewa kwa awamu ya tatu wanafunzi wale waliokosa kujisajili nao wanajaza sasa ikihusishwa wanachuo waliomaliza diploma NT6 Level, na matokeo yao kutoka rasmi mwezi July. Hivo basi tunayatarajia majina kutangazwa rasmi wiki hii au mwishoni mwa mwezi huu, kuhusu website ya TCU kutokufunguka ni kwamba database inapokuwa inawekwa faili zenye Gygabyte kubwa basi access yake inakuwa limited hivo kitumbua kiko jikoni jiandaeni na vikombe vya maziwa kujua chuo gani umepangwa, mie nisistize tu kuwa hakuna chuo cha kata Tanzania hao wanaosema hivo hawajui degree inatafutwaje!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…