Kuna mwanasimba aliyemuelewa huyu Sadio Kanoute?

NguoYaSikuKuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
681
Reaction score
1,020
Sijui kigezo kilichotumika kumleta huyu jamaa Sadio Kanoute.

Wengine watasema alikuwa kiungo bora kwenye mashindano ya CHAN 2019. Lakini huyu jamaa kifupi anachangia kuzamisha sana mtumbwi wa Simba ana bado wanalazamisha kumchezesha. Ni kiungo asiye na kasi na mpira, kumbuka kiungo mkabaji muhimu uwe na kasi kwa mpira wa kisasa.

Haya ndiyo niliyoyaina kwa Sadio Kanoute.
1. Yupo slow sana
2. Sio mzuri kwa mipira mirefu yaani kuhamisha timu.
3. Hana dribbling hawezi kuhold mpira hasa timu ikishambulia au kushambuliwa.
4. Hana commanding power kwa wachezaji wenzake , sio mtu anayeongea ni muda wote yupo kimyaa tu.
5. Passing accuracy yake ni mbovu, nilishuhudia kwenye mechi moja akipoteza pasi zaidi ya tano mfululizo.

Mimi binafsi kilichokuwa kinanikera kwa Mkude ni ile style yake ya backpass nyingi na slowness akiwa na mpira.
Ila.

1. Ana jicho la pasi ndefu na kuhamisha mpira zaidi ya Kanoute.
2. Ana pass accuracy kuliko Kanoute.
3.Anaweza kuhold mpira na dribble kuliko Kanoute.

Kifupi Bora acheze Mkude kuliko Kanoute.

Naombeni mnishawishi nimuelewe, mimi binafsi namuona ni mchezaji wa daraja la kawaida sana.
 
Wanasimba tulieni achane pupa...

Wachezaji wote ni wazuri...

Mnaona mabaya tu kwasabu team haiparform...

Mwakajana hakuna aliye ona udhaifu wa Mugaru ila now kila mnaona...so kuweni na subira..

Mambo yanakuja...

Yanga isiwape presha ni team ya kawaida sana.
 
Kuna kila uwezekano Mo Dewji kajiuzulu Uwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SSC baada ya kugundua kapigwa pesa katika manunuzi ya wachezaji kadhaa pale Msimbazi

Majority ya new signings hawana kiwango na hawakustahili kuichezea Simba. Kanote ni mmojawapo ya hao wachezaji
 
Kibu ni mzuri saana ila ana papara anahitaji wataalamu wa psychologically ili asilazimeahe kufunga yeye ili kuonyesha kuwa yeye ni bora bali aelewe mchezaji anayetoa assist ni bora zaidi ya anayefunga
Amekamia sana kuonesha ubora wake kwa pupa. Atulie aache papara.
 
Mimi naona tumerudi nyuma hatua kumi. New signing zote wametoka ligi za kawaida ukiacha Henock aliyetoka ligi ya Congo.
 
Hebu nisaidie ni mchezaji gani simba walimsaini na ghafla akafanya vizuri...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…